Skip to main content

Glasgow 2014....

Siku ya Pili ya Mashindano ya Jumuiya ya Madola, nipo eneo la Tukio kwa Wiki 2....interested?....me neither!



Kama umewahi kufanya kazi au kutembelea Jiji la London au NY au hata Dar(City Centres sio Keko sijui Masaki huko, nazungumzia "kiini")....ukija Glasgow bana.....ka' sio Jiji, yaani hakujachamgamka kiviiiiiile(ka' Jiji).....




Ila kuna kama "fun fair" kwa kids(sijui wanaitaje bana), nadhani hiki ndicho kitakachonileta huku mara kwa mara.




Michezo imeingiliwa na watu kutoka "Makabatini" bwana, wamefanya watu tushindwe ku-concentrate na Mashindano.....yaani "ukorosho" wao una distract kimtindo....maana wengine tulikuwa tunapenda Mbio na Kuogelea....kuangalia "zile maumbile" za Wakaka pale kati na Miguu (au ni mimi tu nakua pervert wa Kike....hihihihi).





Siku hizi bana mtu unajisikia vibaya hata kuangalia mchezaji, akili kama inahamia kwenye akifanyacho private! Kwani lazima watuambie wao wanalalwa na wanaume/wanawake wenzao?....Mbona sie "tulionyooka" hatuhangaiki kutaarifu Dunia? SOOOOOOO annoying.





Wakianza tu kutoka kwenye Mpira wa Miguu (which nadhani hawatatoka for biz reasons japo kuwa wapo) akyanani vile siangalii tena Kabumbu(si mshabiki, I just penda Mchezo).





Mtuache tubaki tukijiuliza hivi yule ni Mkorosho?....mmh lazima atakuwa Mkorosho, ujue kutokujua jambo na kukufanya ujiulize(kama unao muda huo) kunaongeza mwendo wa siku yako....mara boom saa moja Usiku, watoto wanatakiwa kwenda kulala na siku imeisha!




Speculation is fun.....hujui nini kinaendelea unabaki kuspekyuleti mwishowe unajiona Jinga unaachana na issue nzima.



Nikutakie Mwanzo Mzuri wa Mwisho wa Wiki.



Babai.
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao