Skip to main content

Nipo mtaani kwako, upo home?...

Sipendi hii tabia kwa Moyo Mkunjufu kabisa!!!


Nilikuwa namkimbia rafiki yangu Mghana kwa tabia hii....niambie basi siku moja kabla hujaja kuwa unapanga kuja kwangu....sio unafika Mtaani kwangu au pengine Mlangoni halafu ndio unaniambia kwa Simu!




Sio peke yake, hata ndugu (wa mbali) na jamaa wanatabia hiyo....kuna siku (nikiwa bado Nyumbani) nilimrudisha mtu kwao on next flight....the next Bus bana, hela ya next flight mie ninayo?!!....nikaambiwa nina Roho Mbaya.





Katoka huko Mwanza sijui wapi eti kaja kutafuta Kazi, asa kwanini usituambie mapema tujiandae na Bajeti!....anyway achana na hilo.




Mie huwa sifanyi jambo ambalo najua sipendi kufanyiwa, tatizo linakuja pale Mwenza wako sasa anatabia hiyo....hehehehe Baba Babuu Asali wa Moyo wangu bana anaudhi kweli!!!





Mnaweza mkawa safarini mara akakumbuka fulani anakaa karibu na hapo mnapopumzika labda....ananyanyua simu "eh bwana fulani! Upo nyumbani?....tupo hapa karibu kama vipi tuje kuwasalimia"....aiii! Naudhikaga*(huwa naudhika) sana sababu najua adha yake na siipendi.





Hata nikimwambia ni tabia mbaya wala hana habari, wenyewe wamemzoea. Ila wakitaka kuja kwangu bi Shalilah(hata sijui maana yake), sharti wanambie mapema.....Mwanamke nyumba na Sheria zake nazitunga/weka mie!





Ujue kuna siku mtu hujisikii kukutana na mijitu, alafu boom "nipo hapa, upo home?"


Tabia hizo za kuibuka kwa watu kwa kutoa notisi ya muda mfupi zikanifanya ni-redirect simu zote za ndani to a mobile so hata nikiwa home nasema tu sipo, "mbona umepokea simu ya ndani" nasema nime-redirect simu zote kwenye Simu ya mkononi.



Ustaarabu waja kwa namna nyingi, kutoa taarifa mapema nao ni ustaarabu(unless ni immediate relative then njoo wakati wowote).


Babai.
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao