Skip to main content

Kabla ya Mobile Simu na Net....

Ulikuwa unafanya nini na muda huu unaotumia Simu yako au Mtandao eti?!!


Jinsi Teknolojia inavyozidi kukua ndivyo ambavyo maisha yanazidi kuwa busy na kuhisi muda haukutoshi (Masaa 24 yamekuwa machache).



Binafsi nilichukua hatua ya kutoka Mtandao mmoja wa Jamii na Kujiunga na ambao ni latest one (Mwisho ilikuwa Twitter karibu Miaka 5 iliyopita) hivyo sikuwa kwenye Mitandao Saba ambayo ingenichukulia Muda wangu mwingi.




Kabla ya hapo hakukuwa na Mitandao ya Kijamii, kulikuwa na Forums na Chatrooms pamoja na kuwa nilikuwa na Muda mwingi bado sikujiunga na kila Forum/Chatroom iliyojitokeza.



Hapa juzi nimemsikia Business Woman akisema ameamua kufuta Email address yake na baadhi ya namba za Simu za Ndugu, Jamaa na Marafiki wasio na Mpango (wasiomsaidia kwenye Biz yake) ili aweze ku-focus zaidi kwenye Uzalishaji na Uendelevu wa Kampuni yake.





Anadai kuwa Teknolojia ya Smartphone imesababisha yeye kupoteza muda mwingi kujibu Mails ambazo hazina umuhimu maishani mwake, hivyo akazuia kuzipokea, lakini akawa anapata lawama kila anapokutana na Ndugu, Jamaa na Marafiki....hiyo ikamsukuma kuifutilia mbali "account" yake.





Nimesoma hiyo Wiki mbili baada ya mimi "kupumzika" kwenye ile Blog yangu ingine ambayo husababisha mimi kupokea Mails za kila rangi ya usumbufu na Lawama kwanini sijibu mail "binafsi"(sijui hawaoni kuwa D'hicious sio blog ya kurafikiana)!





Sasa leo hii nina "kajeshi" ka' watu wa Tatu(watoto na Baba yao) ambao ni muhimu maishani mwangu. Wawili kati ya hao (watoto) wanahitaji kufunza HISABATI (nalia sana kila nikifikiria Hisabati).




Nahisi kama muda umefika wa kuifunga ile Blog. Wee unaonaje?


Babai...
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao