Skip to main content

Posts

Showing posts from May 1, 2014

Kilugha kinakera!

Morning/Noon! Lugha za Tanzania zinaingiliana hivyo hazikeri alafu lazima utaambulia maana kwa mbali hasa kama unatetwa. Kuna Mtangazaji "Tiger beibiiii" wa Ebony ya Iringa huwa ananikosha sana akitumbukizia/nogesha kwa kilugha chake, sio Watangazaji wa Dar wamejaa "you know what I mean" "waraaaap" nyiingi....hiyo sio nukta, nimegusia tu. Lugha za Nchi hii bana ayee! Kichina, Kinigeria, Kipolishi, Kizairwaa, Kisomali, Kirusi na nyingine nyingi....zinakera sana (kwasababu sing'amui kitu). Asa ombea umepanda Basi Moja na Mnaija, Mkongo na Mchina, alafu wapigiwe simu kwa wakati mmoja....Utadhani wamekodisha basi kwa ajili yao tu. Sikuhizi nawaelewa sana Wainglishi wanapoonyesha kukerwa unapoongea Kilugha chako....(Sehemu ni wivu as hawajui lugha nyingine hihihihihi). Huwa siongei Kiswahili ninapokuwa kwenye kadamnasi ya watu ambao najua hawaelewi na kama mazungumzo ni nyeti (lazima kilugha ili wengine was

Daktari na Dawa wanazotupa....

Jambo weye? Umewahi kwenda kwa Daktari ili kuongezewa Dawa unazotumia (repeat prescription) Daktari akakubadilishia Dawa akikuambia "hii ni bora zaidi" kuliko hiyo?!!! Unahofia "side effects" lakini Daktari anakuhakikishia kuwa hakuna baya litakalotokea (niligundua kuwa dawa mpya ni Ghali zaidi kuliko ile ya awali). Jana natazama Documentary (yeah am that boring) nkajifunza kuwa hawa Madaktari tunaowaamini wakati mwingine wanatupa Dawa kama majaribio bila sisi kujua. Na wakati mwingine wanakula Deals na Makapuni ya kutengeneza Dawa ili kufanya Dawa husika kuwa popular au kama sehemu ya Uchunguzi. Ile "kama utapata tatizo lolote tafadhali nipigie simu haraka" hiyo ni report muhimu sana kutoka kwako kuhusu dawa husika. Ushindani wa kuuza Dawa kwenye Makampuni hayo ni mkubwa sana, imefikia mahali Madaktari wana-creat "Disorders" na kula Deals na Wafamasia ili kutengeneza Dawa "kutibu/tuliza Disorders&

Wanyumbani na Wanje....

Heri ya Wiki Mpya! Siku hizi wa Nyumbani na wa Nje zimekuwa "jamii" mbili tofauti wakati zamani tulikuwa kitu kimoja ailimradi tu sote tunatoka Nchi mmoja iitwayo Tanzania. Kuna kama kaushindani au kaubaguzi ka chini kwa chini hivi....well, nilishakuambia kuja Nje siku hizi sio deal labda ndio maana wa nje tunadharauliwa hihihihihi. Alafu tunajifanya tunajua sana utatuzi wa matatizo yanayojiri nyumbani wakati wengine hatujagusa huko mwaka wa Tano huu....kazi kufananisha tu "Kwa mfano huku blablabla" sort of people. Pia kuna wale ambao wapo Nyumbani kazi yao kulinganisha pia....wale akina "when I was in London" kind of people...."Hata wenzetu wa Ulaya blablabla" wakati hujawahi kuishi huko au ulikaa si zaidi ya tumiaka 3. Wote hamna tofauti linapokuja suala la kujifanya mnajua utatuzi wa matatizo yanayojiri Tanzania (hasa kijamii, kisiasa na kiuchumi). Sie wenye watoto wadogo haturudi moja kwa moja

Hoarders....

Hello! Mambo! Wadogo zangu wa Kike enzi zile walikuwa wakiniita....wacha ni seme tu bana....najulikana kwetu kama "mchafu" sio kwamba siogi, sishafishi nyumba au kutandika kitanda la hasha! Nilikuwa nafanya hayo yote in my own time....sio ukiamka tu unakimbilia kuosha vyombo(which I hate) au kupiga deki na kupangusa vumbi incase wageni watakuja.... So nilikuwa na-swap kazi hizo na yeyote mwenye zamu ya Kufua au kunyoosha....nazipenda kwavile zinafanywa baadae....pia napenda kusafisha choo/bafu (huwa nasafisha usiku)....hihihihi. Asa siku moja mume wa mimi na mimi tulikuwa tunaangalia kipindi kuhusu Hoarders....hee, mkibaba akaniambia wee mwenyewe ni "hoarder" aiiii niliumiaaaa mpaka nikakaribia kulia! Wacha nianze kubisha(vere mbishi nikiwa na uhakika, tabisha mpaka kesho yake) na kuthibitisha maana ya Hoarders....nikisisitiza kuwa ni Ugonjwa wa Akili. Kesho yake nikaenda "store" nikakutana na Masanduku na M

Lete Ushahidi wa unachoongelea...

Hello DHB/DHW member....year 2003 lazima umezaaka hihihihi maana mie tu niliekua katoto mekuwa kibibi(no, not princess, ni kibibi as in Mzee).....drop me a line please!! Enzi hizo bana, kulikuwa na malimbukeni wa Elimu ya juu kibawoo au niseme Wasongo....ukisema kitu online lazima wakuambie uwape/utoe vielelezo au statistics. Yaani walitufanya sie wa Elimu ya Chini going on to Elimu ya Juu(enzi hizo) tujione "hamna kitu" kabisa, tulinyimwa haki ya Msingi ya kusema tulichojisikia au tulichotaka au kukijua . Ukiongelea kitu bila kuwapa "ushahidi" wanakuambia unaongelea mambo ambayo "unadhani" unayajua, lazima mtu uwe na ushahidi wa kuthibitika kuwa unachozungumzia "umesomea" au unakisoma. Siku hizi aiii unapewa kielelezo cha picha inayotembea na sauti kabisa tena bila kuomba....shukurani kwa Teknolojia na urahisi wa ku-share yale tutakayo/ujisikiayo. Kwaheri kwa sasa. Mapendo tele kwako...