Skip to main content

Posts

Showing posts from June 1, 2014

Michezo ya Utotoni 90s

Jambo! Msita (Mdako), Dama, Marede, "Amina sasa naomba, turudiane...hayo yamekwisha kipenzi changu" yaani kuruka Kamba....don't you miss them au wewe ulikuwa wa Kishua unashinda kubebelea ma VHS ya akina Comando Kipensi....?? Usiseme ulikuwa unacheza Game, enzi hizo Bongo hakukuwa na Games za Tv achilia mbali PCs....Tv zenyewe zimechanganya 1994. Nilikuwa mzuri sana kwenye Marede na Mdako(Msita kwa wale wa pande za Shinyanga na Mwanza). Nikikamata Jiwe kwenye Mdako sikosei....kwenye Marede kila Timu ilinitaka mimi (niligombaniwa). Marede ya kujaza Chupa kwa mchanga niliipenda lakini sikuruhusiwa kuicheza kwasababu ya vumbi(Nilikuwa na Pumu). Ila nilikuwa naibia....kisha narudi ndani nimebanwa....kupumua siwezi....jicho limetoka ka' Ndula(unazijua Ndula weyeeeee)....hehehe. Naishia kuonewa huruma na kupewa na kupewa ile Inhaler, kisha nakuwa nimerudishiwa Uhai.....Nashukuru Imeisha (sijabanwa Tangu nilipofikisha miaka 21).

Heshima kwa Maiti...

Imepotelea wapi? Au ndio kwenda na Wakati? Juzi kati nimekutana na Picha ya Maiti ya Mpendwa wangu....pamoja na familia kufanya kazi ya ziada kuzuia upigaji Picha wa shughuli nzima ya Mazishi achilia mbali Mwili wa Marehemu wa mpendwa wetu zaidi ya alieajiriwa kwa ajili ya kazi hiyo....bado kuna jitu likapiga picha na ku-share online. Kwasababu hana Uhai tena haina maana kapoteza Haki zake kama Mwanadamu mpaka atakapozikwa(Fukiwa). Maiti ingeweza ingejisitiri na kupozi ili apendeza au kutokea vizuri zaidi....pia angechagua ni Picha gani itumike kutangaza Tukio lilipolekea Mauti kumfika. Unapata faida gani ku-publish au ku-share picha ya Maiti?.....kwanini unataka tumkumbuke Marehemu kama Maiti na sio alivyokuwa Hai na mwenye furaha?!! Unaweza kusema naegemea kwa Waingislishi kwa vile naishi huku na wao hawana utaratibu wa kuonyesha Maiti au kuiaga zaidi ya Jeneza na Picha ya Marehemu alipokuwa hai....nia ni kubaki na kumbukumbu ya yeye

Radio za Dini

Hiyaaaaa! Umewahi kuzungumzia Sheria za Dini ya Kiislam dhidi ya Wanawake kwa Binti wa "kisasa" wa Kiislamu ukasikia anavyojitetea!....Hadi huruma. Kuna siku mmoja aliniambia Uislamu hauna budi kubadilika baadhi ya Sheria na kwenda na wakati.....sizungumzii wale Waislamu wa Mwezi wa Ramadhani to Ramadhani....la hasha! Nazungumzia wale Mabinti ambao wanaipenda na kuifuata Imani yako kwa Dhati lakini wanahisi kuna mambo kwenye Sheria ya Dini yao zinawakandamiza. Nimekuwa nasikiliza sana Radio za "Kiislam" (za Kikristo miyeyusho,kazi kuomba Michango tu).....napendezwa sana na Mafundisho yao ya Maisha, kitu pekee kinachonikwaza ni pale wanapozungumzia Wanawake....Mwanamke kwenye Imani ya Kiislam bana....daaah!(Naachia hapa). Radio za Kikristo nazo zimejaa Ushuhuda wa kipuuzi tu yaani....alafu wanaomba Michango kuliko kufundisha wasikilizake wake namna ya kuishi Kikristo.....Maombi ya Michango ya pesa 90%....Shuhuda 7% na 3

Kuchapia...

Ni Sunna....Relax! Enyi Wakaguzi wa Lugha Fasihi sijui Fasaha Mtandaoni mnahitaji kwenda kunywa dawa zenu....(Lazima mna some sort of Mental Disorder). Ailimradi unaelewa kinachozungumziwa au kilichokusudiwa unapaswa kurekebisha kichwani mwako kisha endelea na mambo mengine... Wengine tunachapa/ongea haraka na muda wa kuanza kuhariri hatuna....Mimi binafsi ni Bingwa wa kuchapia....mara nyingi nikisoma (kesho yake) nagundua kuwa nimechapia lakini bado naeleweka. Huwa nachapia hata nikiongea na watu japo sio sana, labda maneno mawili kwa siku....aiiii hebu ngoja kwanza....sasa nina watoto which means naongea zaidi....usikute nachapia zaidi ya maneno 10 kwa siku! Haulipii kusoma na alieandika halipii Kodi kuandika....tulia na furahia uwepo wako Online. Kumcheka mtu kwa vile nimekosea/chapia is bullying/Trolling.....hihihihihi! Happy new Week! Babai... Mapendo tele kwako...