Skip to main content

Posts

Showing posts from July 1, 2014

Kupotea Suna!

Mara ya kwanza kumiliki "SmartPhone" ndio ikawa mwisho wa Mimi kupotea(in my head)....leo 2014 na Tech yote ya Ramani na Gadgets zote zilizopo za "Directions" bado napotea.....Hapo ndio Suna inakuja sasa(sina sababu nyingine). Kwa kawaida nikipotea huwa sioni aibu kumuuliza mtu au kuomba anielekeze....tofauti yangu na wewe ni hivi; huwa sisimamisha mtu yeyote tu, nategea wale ambao sio attractive (at least machoni mwangu). Kwanini nachagua unattractive watu(Wake kwa Waume)? Hata sijui....ila nahisi kama wao ndio wanatoa maelezo vizuri kuliko wale "attractive"....wanakuelekeza utadhani unawatongoza(mie mwanamke, mke na mama nikutongozee nini wee fala...). Naweza nikaenda mwendo mrefu kutoka sehemu niliyopotea mpaka nikutane na unattractive person ndio nimuombe "directions". Nishakuwa stereotyped sana, hivyo wala siogopi kustiriotaipu watu.....ndio maisha...heri umejua kuliko ningekudanganya. Si eti?

Macho yane...

Jana si nilikuambia "nalikizoka" sehemu- sehemu ya Ulaya?....nkaenda kwenye Shopping Centre yao kubwa na wanangu wawili! (Siku zote huwa napita kwa nje tu). Simlituambia wa Ulaya hatuwezi "kulikizoka" Tanzania, sababu tukija huko sio Likizo tena bali tumerudi nyumbani, ni ukweli kabisa (sijui hili limekujaje hapa, tuliache)! Basi humo ndani (shopping centre) Macho yangu yamesifiwa na watu kibawoooo....hee! Mwanamke nikashanga....(Najua nina tumajicho tuzuri ila sio kiviiiiile)! Mkaka mmoja akashindwa kujizua akaniuliza "where are you from"? Nkamwambia "England" hihihihiihi nkaona NOMA! nkasema Tanzania, East Afrika, I have 2 kids and a husband....akasema "are all grown women look like you?....Fit, Nice skin and beautiful eyes?" Nkasema Yes! (Nimeitangaza Tanzania hapo) England hawayaonagi Macho yangu au dharau tu washenzi kabisa wale, mmmh! Ila inawezekana ni u-busy wa Maisha. Watu hawana habari, akili yote ina-focus kwenye £ ili kulipa

Siri...

Unawajua wale akina "nilificha/nilifanya SIRI kwasababu nilikuwa nalinda hisia zako"....."Kwasababu sikutaka kukuumiza" mifano ya watu the shenzi kind of people? Halafu sasa umejua! maumivu ni zaidi kuliko ungejua siku aliyoifanya hiyo siri....well in my case, reaction yangu ni ileile ufiche siri kwa miaka 10 au uniambie masaa machache yaliyopita....AM GONE!! Siri uliyofichwa kwa Miezi/Miaka huuma zaidi kuliko kuambiwa moja kwa moja! The thing is kuendelea kuishi na mtu huyo ni sawa na kuishi maisha ya "Uongo". Usikute hapa nafichwa mambo kibao alafu kimbelembele na-blog hihihihihi, siku nikijua hata kama nimefikisha miaka 50, sisamehi aisee...hii ni karne ya 21 sio Enzi za Yesu!! Aah. Kuna mambo ya kifamilia hupaswi kumueleza mwenza wako unless unajua kabisa yatamu-affect yeye na watoto. Vinginevyo yaache huko huko "familiani". Sasa hizo sio Siri ninazozungumzia hapa, maana hazikuhusu! Si

Karibu, jisikie upo Nyumbani....

Utawekewa "Maeneji" mabaya nyumbani kwako na maukarimu yako yaliyopitiliza yasioyojua mipaka, shauri yako! Unawajua wale wageni wanakuja kwako alafu wanaaza Ziara rasmi ya Chumba hadi Chumba, Droo hadi Droo, wanajipulizia Manukato yako na kujaribishia Viatu na Nguo zako.....WANANIUDHI sana. Wazungu wao huona sifa au sijui ni Kacha yao! Hata sielewi, kama ni mara ya kwanza kufika kwake atakupa Ziara ya nyumba yote mpaka Stoo kwa hiari yao....(Tuwaache). Ujue hapa Duniani bana kila mtu anamikosi yake, shida, raha na tabu zake. Hujui kapita wapi kutegemeana na "Imani" yake ili kujaribu kuiondoa Mikosi (kila mtu na siri yake bana). Siku unamkabidhi Nyumba yako unaanza kuona mambo hayawi mambo. ....usikute "eneji" yangu nzuri kwangu mimi na familia yangu, sasa ukinikabidhi nyumba yako nijisikie ka' kwangu alafu "eneji" yako mbaya ikai-triger "eneji" yangu nzuri na kuzalisha "sumu" yakawa mambo sio mambo usilalamike....Mfano tu