Hujawahi kujiuliza kwanini huyu fulani anapenda kuzungumzia mwanae lakini hajawahi kuweka picha ili na mimi angalau nipate picha ya alivyo kila anapomzungumzia.
Well shauri yako ila najua mie nimeisha jiuliza to the point napata hasira(hihihihi sio hasira bali whys lundo).
Kuna dada mmoja (enzi zile bado nipo kwenye social media) alikuwa ana-share mengi wakati wa Mimba....alimalizia na baby shower na habari ya mtoto kuzaliwa halafu ndio ukawa mwisho.....akawa anamzungumzia tu na kushare zawadi alizompatia kwenye Siku ya kuzaliwa n.k....mapaka leo sijui sura wala rangi ya mwanae......sio muhimu kihivyo lakini muhimu.
So kama mimi enzi nilikuwa nahisi hivyo hakika hata wewe ungependa kuona sura za wananhu si eti eeeh.
Nili-share picha kiasi nilipokuwa kwenye Sosho media so walionifuata wengi wanakumbukumbu kwa mbali ya wanangu walivyo japo sasa wamekua mmno.
Kuna sababu nyingi zinazofanya watu kuzuia picha za watoto wao kuzagaa mitandaoni hasa kama wazazi ni maCeleb.....
.....maana hakuna mzazi anataka kuona comment mbaya kuhusu mwanae hata kama ni za kweli.....au wengine wanahamishia chuki zao kutoka kwa Baba Celeb kwenda kwa mtoto....so unfair.
Kwa sisi wa Ulayani ni tofauti kidogo.....ukishare nyingi unaweza anza kufuatiliwa kwanini wa-share kila pic....mpaka za mtoto anaoga au kujisaidia....unaeza nyang'anywa mwanao kwasababu ya kupitiliza kushea mapicha ya innocent tots bila idhini yao watoto.
Halafu wanapokuwa shule unakamatwa na Policy....kila Shule ina policy yake sasa ikiwa mtoto anasoma Shule ambayo hawataki uweke picha za mtoto Mtandaoni ili kuepuka bulling na misuse sasa au huko mbeleni.....kidogo inakuwa ngumu.
GOOGLE na Tecknology imefanya Dunia kuwa Kijiji.....mtu anaeza kumfuatilia mwanao kwa picha unazoweka na ile kafikisha miaka kadhaa tu anamdaka na uyhibitosho wa Picha zote za utotoni mpaka hapo alipo.
Enzi nasoma Msingi kuna msichana alimkana Mama yake.....kwa vile tulikuwa hatumjui ilikuwa rahisi kumuakini....sasa watoto wa leo watatukana vipi hasa kama Wazazi wenyewe wapuuzi puuzi na habari zetu(sio mimi bana wao khaaa....mie ananijua nani) zimejaa online.
Something like....your dad cheated on his wife with your mum for you to get life(sababu ya wewe kuwepo Duniani was a dirty nanilinhu).....si unawajua funs bana.
Babai.
Comments