Skip to main content

Jipe Changamoto Deilee....

Mambo?
Kama ni mfuatiliaji(mshiriki) kwenye mambo mbali mbali yanayoendelea Online iwe ni kutoa Misada kusaidia wengine, kuhamasisha juu ya Afya, kuelimisha wengine kuhusu issue mbali mbali za Kijamii na hata yale ambayo ni Binafsi.



Utagundua kuwa hayo niliyoyataja hapo juu huwaunganisha watu wote na kuwa kitu kimoja kwenye Suala husika linalofanyika kwa Wiki/Siku husika, Pamoja na kuungana huko bado hutokea kutofautiana na kutokana na "utoto" wa baadhi basi kufarakana hujitokeza na hivyo kufanya baadhi kutengwa, semwa vibaya  hali inayopeleka wengi kuogopa au kukwepa "kushiriki" kwenye hayo mambo ambayo baade hutumika kusuta wengine.....hukufanya hivi tulivyo fanya vile, halafu leo kimbelembele....si unajua?



Sasa ikiwa wewe ni kama mimi(sio mtu wa Drama) na hupendi kujionyesha au hutaki watu wakujuuuuuuue, yeah naandika mengi kuhusu mimi (Kila kitu Mie...got it?)lakini bado hunijui amini nakuambia hihihihihi. Anyway kama wewe upo kama Mie utakuwa na ile tabia ya kujipa Changamoto kivyako kwa faida ya watu wengine.



Changaoto za kujipa zipo Nyingi kuanzia kuchangia Ujenzi wa Choo Kijijini kwenu, Kuajiri Vijana kadhaa Wakati wa Kilimo, Kuchimba Kisima, Kusomesha Sekondari Watoto wa Fukara kila baada ya Miaka 4 n.k. Ili kukamilisha hili hutumii Savings bali unajitahidi ku-cut back matumizi yako ili kufanikisha Changamoto uliojiwekea.



Ukiachilia Mbali hilo, kuna zile Changamoto za kila Mwaka/Mwezi/Wiki ambazo ni za kibinafsi zaidi, na mimi nimeamua kujipa Changamoto ya Mwaka ya kutonunua Tope(Foundation) mpaka nilizonazo ziishe(namna ya kuzimaliza pia ni changamoto ndani ya Changamoto ambayo naifanya weekly).




Pamoja na kuwa tayari nina Changamoto inaendelea nikaona sio mbaya "nikisafisha" Mwili na nikajipa Changamoto ya kukata/ondoa Chumvi kwenye Chakula nilacho kwa Mwezi wote wa Rent, Nilipofanikiwa nikaamua kujipa Changamoto  mpya ya kunywa Maji Mengi kwa Wiki moja ili niweze kufanya unywaji wa Maji kuwa Habit. Kawaida nilikuwa nakunywa 60ml kwa siku, hii ni kutokana na hali ya hewa na unywaji mwingi wa Chai.



Leo namaliza Wiki Moja tangu nianze kunywa Maji 1200ml kwa siku, safari haikuwa rahisi na siku ya Tatu nikaongeza na hivyo nikanywa 3000ml nadhani Mwili ulishtuka na hivyo nikaumwa sana Kichwa(too much water i guess). Siku kata tamaa nikaendelea na 1200mil zangu. Unatakiwa kunywa maji kulingana na Uzito wa Wili wako, kamuone Daktari wako au Kaguge au Pakua App, weka Kilo zako na app itakuambia unatakiwa kunywa mil ngapi kwa Siku ili kuepuka Kifo, yep Majini ni Uhai lakini too  much yachukua Uhai(kifo).



Nilikuwa nakunywa vipi?

Najua unatambua kuwa hupaswi kunywa Maji hayo kwa mkupuo kwani utakuwa bloted na hata kusababisha matatizo mengine ya Kiafya ikiwa ni kuvimba Ubongo, hii ni kutokana na Maji kuwa zaidi kwenye Damu kuliko Chumvi na Sodium. Pia hupaswi kunywa Maji peke yake kwa wiki kwasababu unapata vimiminika vingine kutoka kwenye Chakula na Matunda bila kusahau Chai.



-Nikiamka  tu 6am-Nakunywa 600mil(bila kusafisha Kinywa....heei)
-Dakika 30 kabla ya kifungua kinywa namimina 150ml
-Baada ya kifungua Kinywa namimina 150mil
-Dakika 30 kabla ya Mlo wa mchana nachukua 150mil
-Dakika 30 kabla ya Mlo wa jioni 150mil


Natumai Post hii imekupa mwangaza kiasi kuhusu faida ya kujipa Changamoto  mwenyewe, Unaweza kujiunga na watu wengine kwa support online ila mie ni Loner na Control freak, i am much happier when I do things  my way and all alone.



Shukurani kwa kuichagua Blog hii, naeshimu na kuthamini Muda wako hapa.
Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao