Skip to main content

Juice na Soda husababisha "Homa" zisizoisha kwa Watoto....


Heri ya Mwezi mpya wa May. Mungu abariki kila jema upangalo kufanya(na-sound kama Pastor sasa eti?)!


Umewahi kujiuliza kwanini Mwanao/Wanao huwa na Homa au Vikohozi visivyokwisha? Ukimpeleka Hospitali na kupima Damu na kila kitu majibu ni kuwa hana Malaria wala Typhoid (hatuna huku ila inawezekana ulipo haya Magonjwa yapo) na magonjwa Mengine ya Utotoni. Wahenga...well Bibi yangu alisema "Mwanangu kuwa Uyaone", mie nasema kuwa na Watoto ujifunze!





Wazazi wengi huamini kuwa Soda  husababisha  Watoto kuchangamka kupita kiasi na pengine kukosa usingizi, baadhi huamini kuwa hufanya Watoto kuwa na tabia za ajabu(wabishi,wakahidi, hawakusikilizi, wananguvu kupita kiasi) kutokana na Soda ambayo huwafanya kuwa "high". Sasa hizo ni Soda na zina some sort of "hewa" sio, kwamaana hivyo Juice za kawaida ambazo hazina Sukari ni salama(nilidhani) tena zile ambazo unachanganya na Maji(squash) ndio Bora zaidi(nilijidanganya).




Kuna wakati tulikuwa tukinunua aina Juice ya Matunda"asilia"bila kuongezewa Sukari, maalum kwa Watoto. Matokeo yake (bilakujua) Babuu akawa na Homa zisizokwisha, yaani karibu kila siku Anachemka. Siku moja tulipoenda "Manunuzini" ile Juice haikuwepo in Stock hivyo tukanunua Brand nyingine ambayo ilisema kuwa ni  jutoka kwenye Matunda Halisi aka "Natural" hakuna addictives. Babuu hakuwa na Homa tena. Ziporudi  zile zilizokuwa out of stock tukanunua tele(maana alikuwa akizipenda), Homa zikarudi, hapo ndio nikagundua kuwa Zile Juice zina kitu ambacho sio Salama!



Kama Kacha(kawaida, Utamaduni) nikaenda Gugo, na kuuliza sababu ya juice "husika" kusababisha Mtoto kuchemka/Homa. Nikakutana na "Aspartame" ambayo ni Sweetner wanayoweka kwenye Juice kuongeza Utamu badala ya kutumia Sukari ya Kawaida. Na huu ndio ukawa Mwazo wa mimi kuwa "Mlevi"wa Kusoma Ingredient(Vitu walivyotumia kutengeneza Bidhaa husika). Natumia muda mwingi kusoma "ingredient" zaidi ya kulinganisha Bei.



Nia ya Post hii ni kukupa mwanga kuwa sio Soda tu zinazoweza kufanya Mtoto "achangamke" sana hata zile Juice laini zinazosema "no Sugar added" zinamadhara kwa Watoto kwa namna tofauti. Mwanangu Homa(naturally ni very active), Wengine wanakuwa too High/Over active



Baada ya Muda nikaja gundua lingine, Mwanangu Hapatani(Allergic) na Karanga au anything Nuts....kuwa na Watoto ujifunze eeh! Tulipiga sana Misele kwa Dermatologist nikaja kugundua Mwenyewe kuwa tatizo ni Karanga(nilizila sana nilipokuwa Mjamzito) na Ngozi yake ni Sensitive na hivyo haitaji Hash Soaps,Lotion etc....hii ni Topic ingine(nikumbushe nikusimulie na nikuambie tunatumia nini ku-keep ngozi safi na yenye afya, no miwasho wala ukavu).


Pamoja na kusema hivyo, usitumie Post hii kama Ushauri wa Daktari, Ikiwa Mwanaoa anaugua Homa mara kwa  mara nenda kwa Daktari kwa Ushauri wa kitibabu na Vipimo/Tiba. Lakini pia ondoa vinjwaji ambavyo sio "Asilia".


Unaweza kutengeneza Juice mwenyewe kutokana kwenye Tunda Fresh. Natambua kuwa kila tulacho siku hizi kina Kemikali(sio natural), lakini mpaka sasa hakuna Issue kiafya inayotokana na Maji ya Matunda kutoka Tunda asilia.


Ahsante sana kwa kuichagua Blog hii, tambua kuwa na heshimu na kuthamini Muda wako hapa!

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao