Skip to main content

Jinsi ya kumfanya Mumeo kuwa kama "Romeo" kwa Juliet...



....sio kiviile ila close(I promise)....Jello!

Kama Jojoba ni Hohoba kwanini Hello isiwe Jello?
Ni kawaida kwa wengi kutafuta "namna ya" kupenda, kuridhisha, kuonyesha mapenzi, kujali n.k. Kuna siku Mtu aliniuliza  afanye nini ili Mumewe amuombe radhi? nikashangaa...kuna watu hawajui kuomba Radhi Wenza wao?



Hakika hakuna Kanuni kwenye Maisha ya Ndoa  lakini kuna yale mambo "basic" ambayo ni lazima kila mtu ayajue na kuyafanya/tenda. Mambo hayo huwa tunafunzwa tukiwa angali wadogo, tukianza Shule na kuendelea kuona Wazazi na watu wetu wa karibu wakiyatenda/fanya . Bila kusahau kutukumbusha pale tunaposahau kuyafuata/tenda/fanya. 



Ndio maana siku zote huwa nasema kuwa Mwenza ulienae hivi sasa ni Matokeo ya Malezi/Makuzi yake  bila kusahau Mazingira aliyokulia. Kiongozi kwenye Malezi hayo mambo huwa ni Mama (au Msaidizi mwenye Values kama wewe au bora Zaidi) kwavile ndio huwa anakaa na Mtoto kwa muda mrefu kuliko Baba.



Sasa pamoja na kuwa wengi wetu  hutegemea/dhania kuwa Kila Mwanaume ni lazima awe "loving" kama "Romeo" kwa Juliet, kwamba anakuambia anakipenda mara kadhaa kwa siku kwa aina tofauti ya Maneno, mkiwa mtaani anapachika Mkono kiunoni, anakupandisha garini kabla yeye hajapanda, anakubusu mara kibao kwa siku, anafanya Ngono Kiromansi mara zote mnapohitajiana...Romeo huyo hakulelewa kwenye Mazingira yale yale aliyolelewa Mumeo. Romeo ni yeye na Mumeo ni Mumeo.



Suala muhimu hapo ni kwako wewe kumjua  vema Mumeo kabla hajawa Mumeo, vilevile ni kwako wewe kuwa wazi kwake(usi-settle for less ila usiende overboard)....kama kuna mambo hawezi/hajui kuyafanya na sio muhimu sana kwako basi achana nayo. Mf;- Kutolewa nje kwa jili ya Mlo, Yeye kuosha Vyombo, Kukuimbia, kusema "honey i am hooooome" hihihihi. 



Kuna yale muhimu/basic ambayo ni lazima ajifunze kuyafanya hata kama hawezi,  nayo ni Heshima, Ukweli, Thamini, Shukurani na Kuomba Msamaha/radhi. Ikiwa Mumeo kabla hajawa Mumeo na hujamuweka sawa kwenye hayo basi Ndoa yako itakuwa Chungu...utahisi kuwa Ndoa yenu ni ya Mtu mmoja na utakuwa Mpweke Ndoani. Utahisi kumpenda Mumeo lakini hutopendezwa nae Siku 305 kati ya zile 365 za Mwaka!....je unaweza kuishi na Mtu anaekuudhi kwa Muda huo wote wa Maisha yako?



Sie wa "kizamani" tulifundwa kuwa Mke anaweza kuchukua nafasi ya "Mama" kwenye kumuweka sawa Mumewe, ila sasa unapomfunza Mumeo yale muhimu ambayo Mama yake  labda hakutilia maanani hupaswi kuwa kama Mama yake kweli na yeye kuwa Mtoto  wako bali unapaswa kufikisha "Somo" kivingine ukijitumia wewe kama mwenye hitaji la "tabia njema" kutoka kwake Mumeo Mpenzi.



Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa Wanaume hawafanyi mambo yale yale ambayo wewe unadhani ndio Kupendwa na  kwamba kila Mwanamke  anapata "Tamu" ya "Romeo" kwa Juliet. Kuna Wanaume ni Wapenzi wazuri sana lakini hawajui kusema "Nakupenda" kila siku, hawajui kusema "samahani/nisamehe" kila wanapokukosea, hawajui kuwa Romantiki.....wana namna zao tofauti-tofauti za kufikisha ujumbe kuwa wanakupenda, wanaomba msamaha na kuromantika.



Siwajui Wanaume wote Duniani ila "I lived" hihihihi so nitakupa Uzoefu wangu. Tafadhali usikose kunitembelea tena ili ujue ni namna gani hasa baadhi ya Wanaume hufikisha ujumbe uleule wa kiRomeo bila kuwa kama Romeo.


Nathamini na kuheshimu Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao