Skip to main content

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mumeo ajihisi "Mfalme"....

Waliposema "ajihisi Mfalme" hawakumanisha akutawale na kukutumikisha wewe Mkewe kama Mtumwa wake na hivyo kukosa sauti na kubaki "Ndio bwana", bali kufurahia maisha ya Ndoa na hivyo kurudisha ufanyao ili na wewe ujihisi "Malkia"......Heri ya Mwaka mpya 2017!!


Mie kama Mwanandoa wa "Kitambo" sasa nimeamua Mwaka huu kurudisha Heshima ya Ndoa baada ya kuona kuwa watu wanapotosha na  hivyo Ndoa kuonekana kuwa ni Kazi...well ni Kazi ya pili baada ya ile uifanyayo kukupatia Kipato au ya Tatu ikiwa mna watoto, lakini sio Kazi kwamba ni ngumu na ukibaki humo basi wewe ni Shujaa. Hapana!


Upotoshaji huo unapelekea baadhi ya watu waliokwisha "onja" Ndoa na baadae kuharibika kuchekwa/shangawa kwanini wanarudi tena Ndoani(na watu mwingine) wakati tayari wanajua "maumivu" ya Ndoa....Vijana wamekuwa wakiiogopa Ndoa.


Kwasababu Ndoa moja imeharibika haina maana zote zitakuwa kama hiyo iliyopita. kumbuka watu wanatofautiana na pia kuna baadhi wanaamini katika Mapenzi na Ndoa, wanapenda kuwa kwenye Ndoa na hivyo hawaogopi kujaribu tena na kufanya mabadiliko.


Ndoa ni mtindo wa Maisha mzuri sana tu, hasa ikiwa wote wawili mlijiandaa kuungana kuwa kitu kimoja, mpo tayari kujifunza, kushirikiana, kuwajibika(fanyia kazi Ndoa yenu) na Makubaliano yenu hayo yaliegemea zaidi Upendo na Urafiki....sio Elimu, Pesa au Mafanikio yenu au  Familia zenu(inasaidia lakini sio lazima).


Wengi huamini kuwa Wanaume ni wagumu sana kuridhishwa lakini kwa Uzoefu wangu uliochanganyika na "common sense" Wanaume are very simple ukiwajulia. Aachana na hili, twende kwenye ku-Mflame-nisha Mumeo sasa.



Kwa kawaida kila Mwanaume(Mume) huwa  na yake apendayo  kufanyiwa na hivyo kujihisi ni "Mfalme" kwasababu Binadamu tunatofautiana, lakini pia kuna yale mambo ambayo ni ya kiujumla. Kwamba haijalishi ni aina gani ya Mwanaume...ukimfanyia yafuatayo(kama hujawahi kuyafanya) hakika utamfanya awahi kurudi Nyumbani kila siku na kutaka kuacha Kazi zake ili abaki nawe nyumbani(halafu sijui mtakula nini?):-


-Muweke Mungu wenu karibu(inategemea na Imani zenu), Ombeni pamoja na umuombee yeye zaidi  kuliko kujiombea wewe mwenyewe.


-Onyesha unajali, thamini, shukuru na kutambua Juhudi zake kwenye shughuli zake za kila siku za kuwaingizia Kipato. Mfanye awe Shujaa wako hata kama unaingiza Pesa nyingi zaidi yake au zaidi ya Baba yako.


-Akitoka, mcheck kujua kama yupo Salama, kwa kawaida utakuwa unajua kaenda wapi (lazima atakuambia)na atakuwa huko kwa Muda gani (+ Usafiri). Mfano kwenda na kurudi ni Dakika 40 nzima, akakuambia atakuwa Pub mpaka Mpira Uishe then usim-check mpaka Mpira uishe. again kwa kawaida atakujulisha kuwa sasa anatoka Pub n.k.


-Lianzishe angalau mara 3 kwa Wiki(inategemea mnafanya mara ngapi kwa Wiki, lianzishe mara nyingi zaidi kuliko yeye), Hapana Mumeo hawazi  kuhusu kufanya mapenzi muda wote na pengine anaweza kukuambia kuwa "kufanya mapenzi sio lazima" lakini ni Muhimu...hapo anamaanisha kuna siku/wakati hajisikii laikini ukimuonyesha njia basi atakufuata  na atamaliza safari na wewe(kama sio kabla yako).



-Tengeneza Mazingira ya Amani hapo Nyumbani, kwa maana ya kujifunza kudhibiti au Punguza Kisirani(zijue Tarehe zako  na utafute mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya Homono unapokaribia Hedhi na pengine Wakati wa Hedhi), sio rahisi lakini inawezekana.


-Amka nae Asubuhi na umuandalie Kifungua kinywa au kama Usingizi wako ni Muhimu zaidi(kama mimi) basi muandalie Chakula cha Mchana ambacho atakula akiwa Kazini. Kwa wale ambao labda hili ni gumu  kutokana na Mazingira au Hali ya Hewa basi Muandalie Nguo za kuvaa kabla ya Siku husika.


-Toa Mkando, Mkande Mumeo mara baada ya kushusha "mabegi" yake ya Kazini(kama unapokea, basi pokea, mie huwa sipokei), mjulie hali huku unamkanda maeneo ya Mabegani na mgongoni, najua kama mna watoto watakuja na kutaka kufanya ufanyavyo kwa Baba yao. Usiwafukuze, waache wajifunze.

-Onyesha kuwa unampenda bila kumwambia unampenda, unaweza kutumia Busu, Kumkumbatia kwa namna ambayo inasema nahitaji uwepo wako, kumpikia vizuri, jinsi unavyo mtazama n.k


-Achana na Mambo ya Zamu yako kuosha vyombo sijui kupika au kuogesha Watoto n.k na badala yake anza kufanya kitu halafu muombe aje/aende kukusaidia kufanya jambo lingine. Jifunze kuzungumza/Wasiliana zaidi kuliko kulalamika.


-Anapokuwa  na Watoto usimuingilie, kumbuka kuna aina ya Kimalezi mnafanya pamoja kama Wazazi (Timu) lakini pia kuna baadhi huwa unafanya kama Mama, sasa muache na yeye afanye kama Baba. Kila Mzazi anasehemu yake maalum na ya kipekee kwenye maisha ya Mtoto/Watoto.



-Jitahidi kufanya Tendo kila Asubuhi, hii ni tofauti na namba 3 ya "Kulianzisha"...hii haihesabiki kwasababu huwa Kasimama tu na sio kwamba anataka Tendo, lakini ukimgusa/kumbatia lazma ata-respond kivingine au wewe mwenyewe Ukiguswa na kitu kigumu asubuhi utatamani iingie mahala. Halafu sababu nyingine inayofanya "cha asubuhi" kisihesabike ni kwamba wewe na yeye actully mna kuwa sleepy and lazy hihihihihi. Hii ni Salamu tu.


-Usafi wa Nyumba(Mazingira), na wewe mwenyewe kujipenda/pendeza.


Nikutakie siku Njema, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Bai bai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao