Skip to main content

Kama Mumeo anakupenda hatoruhusu ufanye haya...


Kutokana na wakati tuliopo ambapo  kuna "informations" nyingi kuhusu nini hasa Mwanamke anapaswa kufanya au kuwa na hivyo kuibua kukanganyana na kudanganyana kuliko wakati wowote ule wa maisha ya Mwanadamu(nimeongeza chumvi, sijui historia ya Mwanamke kabla ya 1900). Hata hivyo bado haiondoi  ukweli kuwa kuwa Mwanamke  mbele ya Wanawake wa kisasa ni Kazi ya Ziada.



Mara nyingi sie(wewe na wenzio) wa Kisasa huwa tunaambiana kuwa mwanaume hana haki juu ya mwili wako au uamuzi wako wa nini unataka kufanya na mwili wako(mavazi/Urembo) which it is true  kama ni Mpitaji(boyfriend) lakini ukiwa  kwenye Ndoa/Uhusiano Mwanaume kuonyesha kuwa anajali nini unaweka juu ya mwili wako ni dalili kuwa mwanaume huyo anakupenda na sio kwamba hajiamini au anahofua kuibiwa.



Wengi mnadanganyana kuwa Mume(au Mume mtarajiwa) akikukataza usifanye mambo kadhaa ni kuwa anaku-control, Nyanyasa au ni Dikteta kwenye uhusiano wenu. Tunasahau kuwa yeye ni mwanaume na hivyo anajua ni namna gani Wanaume wanavyotuona, wanavyotuchukulia tofauti na sisi wanawake tunavyojiona/chukulia.


Mwenza wako anakupenda ikiwa haruhusu yafuatayo;-

*Utoke peke yako(au na Watoto kama mnao) ukiwa umevaa nguo fupi/zinazoonyesha baadhi ya maeneo ya mwili wako ambayo yanavutia. Ukibisha/lalamika ooh "ulinikuta nikivaa hivi na ukanipenda, niache usinibadilishe". Atakubali na atasisitiza uvae hivyo ukiwa nae au ukiwa nyumbani.

Yeye kuweka zuio hilo sio kwamba hajiamini  kama unavyodhani bali ni kujali usalama wako  na kuepusha adha ya Wanaume wengine kukukosea/shushia heshima(miluzi, kutoa maneno ya kukutamani au kukufuata/shika).


*Ulale usiku mzima ukiwa na hasira, hata kama umewahi kulala kabla yake atahakikisha anakuweka karibu ili ujihisi "protected", sio mara zote ukiamka mikononi mwake baada ya kukasirika ni kwamba anataka Ngono. Wakati mwingineni kuomba msamaha na wakati mwingine ni kukulinda au vyote.


*Kupoteza mvyuto wako, hatokwenda kulalamika kwa watu kuwa umekuwa mchafu au hujipendi tena tangu umejifungua watoto wenu bali atakukumbusha mf; "Mke wangu enzi ulikuwa unajipenda sana, ulikuwa hutoki nje bila kujiremba, namtaka mke wangu yule wa enzi" na atakusaidia kukabiliana na majukumu ya nyumbani na mtoto ili upate muda wa kujijali na kujirudishia mvuto wako tena au zaidi ya ulivyokuwa kabla ya Mtoto kuzaliwa.


*Ujishushe, mf; Ki-career au kimuonekano. Ukilalamika kuwa umekuwa sio "smart" tena na pengine umekuwa sio "ambitious"  tena labda ya kukaa nyumbani muda mrefu(Likizo ya Uzazi), yeye atakupa wazo la ama kubadili career(rudi shule), kamwe hatokuambia "natengeneza pesa za kutosha, au nitaongeza huitaji kurudi kazini". Ukiamua kuwa mama wa nyumbani itakuwa ni wewe binafsi.


Ukilalamika kuwa umenenepa/konda nakupoteza shape  na hupendi ulivyo...kamwe hatokuambia "fanya mazoezi upungue au "kula unenepe" atakuambia na  kukuhakikishia kwamba yeye haoni tofauti na uache upuuzi(kujishusha).


Ukisisitiza sana(labda kwa vile kweli unajisikia ovyo sababu hujazoea mabadiliko ya mwili wako) basi atasema "kama ni muhimu kwako  basi kupungua/nenepa ila kwangu you look sexier after kids"..


*Mtu yeyote kukushushia Heshima hata kama ni Mama yake, achiliambali ndugu na marafiki. Pengine anaweza asioneshe hivyo moja kwa moja lakini mara zote atakuwa upande wako na kujaribu kukulinda na kukuondoa sehemu ya tukio. Ata-deal na watu wake na kuwaonya kuwa hataki kuona wanakushushia heshima.


Mumeo anaku-control, Nyanyasa au ni Dikteta ikiwa tu;-

Aanakukataza usiwe na marafiki(wazuri), usitembelee Ndugu, Usiunguze chakula hata kwa bahati mbaya, anakupiga, anakutukana, hakuheshimu mbele ya Ndugu zake, hafanyi mapenzi na wewe(anafanya ngono tu), hataki ujitegemee Kiuchumi, hajali career yako n.k.



Ahsante kwa kuichagua Blog hii, tambua kuwa nathamini muda wako hapa.
Bai.

Comments

Unknown said…
Hakika ni ujumbe mzuri sana. Unastahili pongezi mwandishi.
Unknown said…
This comment has been removed by the author.
Unknown said…
Asante sana dada yangu, Naomba unisaidie nipate yale mafundisho yako ya kwenye Blog ya dinahicious - Relation ship & love
Unknown said…
Hellow! Nimekuelewa

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao