Skip to main content

Nguzo 5 za Mahusiano...Heshima kwa Mumeo.

Nilikuacha solemba eti, natumai upo salama,..mie mzima kabisa ahsante kwa kujali.




Bila shaka unewahi kuona/soma/sikia watu wakisema "Mwanaume haitaji kupendwa bali kuheshiniwa", kwamba Heshima kwake ndio kupendwa...lies the Internet tells.



Mwanaume anahitaji vyote, Heshima na kupendwa....ila ukifikiria kiundani(inategemea na situation iliyokufanya ushushe heshima kwake ) kumpenda Mume wako bila kumheshimu ni ngumu. Acha kufikiria kiundani.




Pengine Mumeo amewahi kukuambia kuwa anahisi kuwa huna heshima kwake...halafu ukang'aka na kudai sio kweli, kwamba mbona unamheshimu sana tu!




Heshima kwa Mwanaume(Mumeo) ni tofauti na vile unamuacha anajiachia kwenye Internet/Bar na wadada wengine, kutopinga maamuzi yake hata kama ni mabaya/hatarishi, kutokuvaa mavazi fulani n.k.



Hivi ndio unavyopaswa kumheshimu Mumeo ukiachilia mbali kumsikiliza pia usizungumzie mapungufu yake kwa watu wengine hata kama ni Mama yako.



Thamini Ndoa yenu (sio kuishi kwa mazoea) na ikitoke mmepishana na kugongana/zozana chunga Ulimi wako na usitumie Lugha/maneno ya kudhalilisha.



Ikitokea amekushirikisha kwenye jambo la familia na akakupa nafasi ya kufanya uamuzi....onyesha kumuamini yeye kufanya uamuzi huo kisha subiri majibu, sio kurudi na kuanza kumbugudhi na maswali.




Badala ya kwenda kwenye Social media/kwa Rafikizo/Wazazi kuomba Ushauri, omba ushauri kwa Mumeo. Pengine Mumeo sio mshauri mzuri kwenye baadhi ya mambo(inategemea na Upeo/Elimu/Uzoefu) bado mmpe hiyo heshima.



Akiamua kusaidia kwenye suala fulani hapo nyumbani muamini na muache afanye mpaka mwisho....unless otherwise atakuomba msaada, usiingilie au kukosoa akifanyacho.


Ni kawaida kwa Mumeo kukataa adharani kuwa ahitaji kusifiwa, kupewa attention au kuhakikishiwa Penzi ulilo nalo kwao. Ukweli ni kwamba hawa viumbe wanahitaji kusifiwa kama vile sisi tunavyopenda tofauti wqo hawahitaji mara nyingi kama sisi.



Sifia mumeo akitokelezea(pendeza), akikamilisha jambo(kubwa au dogo),  mhakikishie kuwa unampenda na hakuna mtu atachukua nafasi yake(kwa vitendo pia)



Je unajiheshimu na unamheshimu Mkeo ili akuheshimu au nikukumbushe pia?


Muda wako hapa ni thamani kubwa kwangu, ahsante.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao