Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mkeo

Namna ya Kumshukuru Mumeo bila kusema "Ahsante".

Ukiachilia mbali(naipenda hii msemo) kuwa Ahsante ni "common" kitu ambacho kinaondoa uzito na maana yake, pia neno hilo ni rahisi na kila mtu anaweza kuambiwa bila kumaanisha. Mumeo sio mmoja ya hao watu, Mumeo ana umuhimu na uzito tofauti na watu wengine wote Maishani mwako(ukute ni mimi tu ndio nahisi hivyo).   Sasa kuanzia leo acha kukimbilia Ahsante kwenye kila jambo analokufanyia kama Mkewe na mlezi wa Familia(watoto wenu) yake.  Moja, Wakati mwingine mpikie/andalie chakula/kinywaji anachokipenda. Mpokee kama vile wanao wanavyompokea(bila kusema babaaa)....hiyo Pili. Shikamaneni hivi ktk Ndoa. Tatu, akikuudhi au ukiudhika na mambo mengine(unakaribia Hedhi) usimfanye alipe, hasa pale anapofika Nyumbani kutoka Kazini. Jaribu kumjulia hali, kumuacha apumzike na kisha ongea nae vizuri na kwa upendo/heshima. Nne, Ilinde Ndoa yenu pale ambapo mambo yqmegona kuendi vema, mfano Kapoteza Kazi/Tenda/Biashara imabuma, badala ya kumpa Moyo, Matumaini na Ushirikiano....we

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mkeo ajihisi Malkia...

...Mengi ni yaleyale yanajirudia.....kukumbushana sio mbaya, kwavile tunatofautiana ni wazi kuwa Mkeo atakuwa  na vijimambo vyake ambavyo anapenda kufanyiwa ili kujihisi kuwa yeye ni "Malkia". Umalkia ninao uzungumzia hapa sio ule wa kuishi kwenye Jumba kubwa zuri lililojaa watumishi au kumfanya Mumeo kuwa Mtumwa kwako....la asha! Habari gani? Kwa kawaida Wanawake(wake) huwa na tabia ya kujitahidi kuwa Wake wema, tunafanya mengi sana kwenye Ndoa(au Uhusiano) na Familia(kama mmebarikiwa Watoto) wakati mwingine kama sio mara zote huwa tunasahau kuwa nasi pia tunahitaji kujisikia kama ambavyo tunawafanya Waume zetu kujihisi Wafalme. Soma Jinsi ya kumfanya Mumeo ajihisi Mfalme  kama uliikosa. Kama kawaida kwenye haya mambo hakuna Kanuni hivyo jaribu haya kama hujawahi na hakikisha unamsoma Mkeo vizuri ili kujua ni kitu gani hasa anahitaji kutoka kwako kama Mumewe. -Pamoja na kuwa anapesa zake, mgawie kiasi cha Pesa  zako bila sababu.....weka mahali ambapo ataziona kwa

Jinsi ya kumfanya Mumeo kuwa kama "Romeo" kwa Juliet...

....sio kiviile ila close(I promise)....Jello! Kama Jojoba ni Hohoba kwanini Hello isiwe Jello? Ni kawaida kwa wengi kutafuta "namna ya" kupenda, kuridhisha, kuonyesha mapenzi, kujali n.k. Kuna siku Mtu aliniuliza  afanye nini ili Mumewe amuombe radhi? nikashangaa...kuna watu hawajui kuomba Radhi Wenza wao? Hakika hakuna Kanuni kwenye Maisha ya Ndoa  lakini kuna yale mambo "basic" ambayo ni lazima kila mtu ayajue na kuyafanya/tenda. Mambo hayo huwa tunafunzwa tukiwa angali wadogo, tukianza Shule na kuendelea kuona Wazazi na watu wetu wa karibu wakiyatenda/fanya . Bila kusahau kutukumbusha pale tunaposahau kuyafuata/tenda/fanya.  Ndio maana siku zote huwa nasema kuwa Mwenza ulienae hivi sasa ni Matokeo ya Malezi/Makuzi yake  bila kusahau Mazingira aliyokulia. Kiongozi kwenye Malezi hayo mambo huwa ni Mama (au Msaidizi mwenye Values kama wewe au bora Zaidi) kwavile ndio huwa anakaa na Mtoto kwa muda mrefu kuliko Baba. Sasa pamoja na