Skip to main content

Posts

Showing posts with the label nakupenda

Sio lazima wote tuseme "Nakupenda"...

...halafu inatumika ovyo sana mpaka imeanza kupoteza Maana kwa Kiswahili(hatuna "like" au hatutaki kutumia kupendezwa) na kwa Kiinglishi. Mtu humjui...ndio kwanza mmekutana, baada ya  kubadilishana Salamu, mnaagana na kuambiana "nakupenda".....wengine mnakutana tu anakuambia "Jamani Dada nakupenda". Hujambo lakini? Pia kuna wale Ndugu...."nawapenda kweli wanangu(yaani wanao)"...akiishi nao masaa 24 lazma abadili usemi wake(au hisia zake). Pamoja na kusem ahivyo bado Uzito wa neno Nakupenda upo palepale....mtu akikuambia hivyo lazima karoho karuke kwa Mshangao au kwa Uoga(kama mna-date)....Kama nilivyoahidi kutoka Post iliyopita (bofya hapa  ) leo tukumbushane namna tofauti ya kusema "nakupenda" bila kusema neno hilo. Umewahi kuambiwa nakupenda na Mke/Mume wako ukaangua Kicheko halafu unajiuliza Kasoma Blog gani leo? hihihihihi au ni Mimi tu!! sio kwamba neno hilo linachekesha bali huwa hulisikii  kutoka kwake. Wapo ambao hu

Jinsi ya kumfanya Mumeo kuwa kama "Romeo" kwa Juliet...

....sio kiviile ila close(I promise)....Jello! Kama Jojoba ni Hohoba kwanini Hello isiwe Jello? Ni kawaida kwa wengi kutafuta "namna ya" kupenda, kuridhisha, kuonyesha mapenzi, kujali n.k. Kuna siku Mtu aliniuliza  afanye nini ili Mumewe amuombe radhi? nikashangaa...kuna watu hawajui kuomba Radhi Wenza wao? Hakika hakuna Kanuni kwenye Maisha ya Ndoa  lakini kuna yale mambo "basic" ambayo ni lazima kila mtu ayajue na kuyafanya/tenda. Mambo hayo huwa tunafunzwa tukiwa angali wadogo, tukianza Shule na kuendelea kuona Wazazi na watu wetu wa karibu wakiyatenda/fanya . Bila kusahau kutukumbusha pale tunaposahau kuyafuata/tenda/fanya.  Ndio maana siku zote huwa nasema kuwa Mwenza ulienae hivi sasa ni Matokeo ya Malezi/Makuzi yake  bila kusahau Mazingira aliyokulia. Kiongozi kwenye Malezi hayo mambo huwa ni Mama (au Msaidizi mwenye Values kama wewe au bora Zaidi) kwavile ndio huwa anakaa na Mtoto kwa muda mrefu kuliko Baba. Sasa pamoja na