Skip to main content

Posts

Kukabiliana na Mwenza/Mpenzi "mpya" baada ya Miaka kadhaa...

....kwa maana ya yeye kubadilika/shwa na "Rafiki" zake kama niliyogusia Post iliyopita, ikiwa hukuisoma basi bonyeza hapa . Upo salama lakini?....twenzetu! Kwanza kabisa usimwambie kuwa umebadilika, lakini akikujia na mambo mapya ambayo awali hakuwa akipenda/fuatlia then hoji kulikoni? mf: tangu lini Mpenzi unatazama Eastenders? Hee siku hizi unafuatilia hiki/kile? hii itamfanya atambue kuwa unaona mabadiliko. Pili, Jiweke mbali, yaani mbaaaaaali na hao/huyo "Rafiki" unaedhani ana/amembadilisha Mwenza/Mpenzi wako. Usimuulizie, akianza kukupa stori bila kutaja jina la Mhusika, wewe sema tu "tunamzungumzia John"(taja jina la huyo rafikie mpya)? Halafu onyesha kuwa huna "interest" ya kujua zaidi.(hii itafikisha ujumbe na hivyo kuacha stori za huyo mtu/watu). Tatu, Ataanza kutaka kukutanisha wewe na huyo "Rafiki" kwa kisingizio chochote tu, kuanzia "ametualika kama familia" au "anataka kuja kututembelea ili awaone