Skip to main content

Posts

Showing posts from April 1, 2014

Nywele....

Baada ya kujifungua Barack na kupoteza nywele za kutosha, nikavumilia mpaka nilipomaliza kunyonyesha. Niliposhika Mimba ya Iman nikaamua kukata nywele hivyo nimekuwa na nywele fupi kwa miaka 2. Siku moja nika-google kujua "Tiba" ya nywele zangu "kumwagika" kutokana na kunyonyesha(mabadiliko ya Homono). Nikakutana na Vlogs za hair journey bana...hee! Nikagundua mafuta yanaitwa Castor (mafuta ya Nyonyo) mwanamke si nikakurupuka....nikawa naosha nywele kila siku na kupaka Mafuta ya nyoyo + leave in + hair cream za kutosha, Wacha nywele ziendelee kukatika mpaka nikawa kipara hihihihihi (I was crying actually). Nikaendelea kufanya Uchunguzi kwa kusoma na kusikiliza Shuhuda za watu nikagundua kuwa nakosea na nywele zangu zilikuwa zinalainika zaidi(too much moisture) bila kupata nguvu kutoka kwenye Protein (nywele zinahitaji balance ya vyote). Ndio nikakutana na wadada wakitoa shuhuda kuhusu Aphoghee Step 2 treatment ambayo unatu

Matumizi ya Tablets kwa watoto....

Mambo! Nitakuwa naandika chochote kinachonijia kichwani kwa wakati huo.....kuanzia malezi ya wanangu, habari itakayogusa Mtima wangu (usijali sio habari za Tz) na siku husika kwa ujumla. Hali ya hewa leo ni ya Unyevu na Mvua kwa mbali, Wataalam na wachunguzi wa huku wanalalama kuwa watoto wasitumie Tablets kwa vile zinawafanya wasiweze kutumia mikono kuandika au kuchora kama ilivyokua kwetu enzi zile. Lakini Enzi zetu si zimepita? hizi enzi zao waacheni ila tuwe responsible na wanachokifanya kwenye Tables, Fundisha mwanao....usitegemee mtu mwingine (Yaya/Mwalimu) akufundishie just because you pay them to do so. kwaheri kwa sasa.