Tuesday, 31 March 2015

Jikubali, Jipende Jiamini so they say....

Habariiii!

Baadhi huitaji support ili waweze kujikubali kujipenda na kujiamini halafu wengine tumezaliwa hivyo.....si vema kukurupuka na kumwambia mtu lazima ujiamini bwana blablabla.....sio chee kama udhaniavyo.

Ni rahisi kujipenda, kujikubali na kujiamini angalau ukiwa umefikisha miaka 25(in my head umri huo ndio unaanza kujitambua na kujijua....unakuwa umekua).

Mara zote Binti unapenda kuchukia baadhi ya vitu kwenye mwili wako hasa kipindi cha Kubalehe(tunabadilika). Huwa ni ngumu sana kukabiliana na mabadiliko ya ndani na nje ya mwili.....kiakili na kihisia.

Kipindi hiki unaanza kujiona MZURI leo basi linapokuja suala la kuagizwa Dukani wewe ni wa kwanza kutaka kwenda ili "wakuone" si wajua kale ka atensheni ka wavulana kanakokusaidia kujua ujinsia wako? Kanakuwaga enjoyable sana......halafu kesho unakuwa MBAYA unagoma hata kwenda Shule unasingizia unaumwa er Macho (that was me).

Ukifikia miaka 25 mabadiliko yanakuwa yameseto na kilichobaki ni kunenepa au kukonda. Unaanza kugundua your best bits mwilini mwako na kuzipenda zaidi ili kuficha zile usizozipenda.

Ukifika miaka 30 na upo tayari kuwa Mama na ukashika Mimba na ukafanikiwa kuzaa aiiiiii unaanza upya au unarudia ile miaka ileeee ulipobalehe......wakati huu ni mgumu sababu mwili umekomaa hivyo hata mazoezi huchukua Muda kutoa matokeo mazuri na ya haraka.

My best bits ni Mwili wangu wote na Macho.....sipendi Kucha zangu za Miguuni pia Mikono kwa nyuma(ya kukamatia sio arms) inaniudhiiiii lakini ndio yangu sina budi kuitunza japo imejikunja oh my Meno too hihihihihi.

Sasa nimegundua kuwa watu wanatumia Vipodozi ili kufungua Macho na pengine kuyafanya yawe makubwa.....kwa kifupi hawapendi macho yao yalivyo bila make up.


Mie ninamajicho makubwa (in my head) na ninayapenda sana tu ila tatizo ni kuwa kila mtu anajaribu kuwa na macho kama yangu(natania) ili niwe tofauti na mimi natumia vipodozi kuyapunguza.

Babai.

Wanaume wanaopenda Natural Beauty....

Lakini bado wanavaa Nguo.....waogope sana!

Kwanza ni kwanini hasa wanaume wanapenda kufuatilia masuala ya Urembo wa Wanawake au Mavazi ambayo hayawahusu? Jibu: Wanaogopa gharama au roho mbaya bin Mfumo Dume.


Mwanamke anakuwa judged muda wote kwa maisha yake yote.....hata mimi nahukumu wanawake wenzangu na mimi mwenyewe lakini hapo hapo huwa najaribu kuelewa kwanini wapo hivyo walivyo(ukiachilia mbali Uwezo wa kifedha) kwasababu najua UANAMKE una issues zake ambazo mwanaume hawezi kuzielewa.


Kutokana na kuwa judged muonekano wa Uso/Sura ni muhimu kuliko sehemu nyingine za mwili ambazo anaweza kuziziba kwa kuvaa nguo.


Mwanamke anapendezeshwa kwa Vipodozi, Mavazi, Vito vya Thamani na Manukato. Ili mwanamke apendeze inabidi awe msafi na ili awe msafi ni lazima aitunze Ngozi yake, Kucha na Nywele......hivi vyote ni gharama.Unawajua wale wakibaba wanaopenda independent women with natural beauty?So that they can spend their money on others while you (independent woman)pay Bills na unachuro byuti wako.....ayiiiiiii napoteza track!!!


Mwanamke anaweza kutanua matawi ya Urembo wake kulingana na miaka au Fashion na hivyo kuongezea pale anapohisi panahitaji ongezo kwa muda mfupi.


Mavazi na kujipamba au kujiremba ni moja ya sehemu muhimu sana kwenye maisha ya baadhi ya Wanawake kwani huwaongezea hali ya kujiamini na wengine wanapata furaha moyoni kwa kupata muda wa peke yake kujiangalia kwenye kioo akijifunza namna ya kuongeza urembo alionao kwa Muda.


Sasa Manabii, Mahimamu na Makasisi wa Kiume ndio imekuwa Topic siku hizi......badala ya kutangaza neno la Mungu au kuelimisha watu kuhusu Imani ya Dini husika wao wanazungumzia mavazi na Urembo wa Wanawake.


Halafu mikimama inayopenda kuwa nachuro(hawapaki hata mafuta ngozini eti sababu Waume wao wanapenda unachuro) ndio washangiliaji wakuu.


Stori time: Once aponi muda nilikuwa napenda kuwa nachuro byuti bana mpaka siku  moja Konda aliponiita Uncle......"Oyaa anko ajasti kidogo basi" sababu nilikuwa nanywele fupi....halafu nimepiga shati (la shule) kubwa so Matiti hayaonekani......nililiaaa mpaka nilipofika nyumbani.


Ndio ikawa siku ya kwanza kupaka Uwanja kwenye water line na kusuka(Baba alikataza kusuka eti napoteza muda ila kilio changu kilimfanya aniruhusu kusuka) hihihihi.....I still look like my Dad's bro aka Uncle though.

Babai.

Tuesday, 24 March 2015

Ile Manukato ya Kiume uitakayo...

Mambo?

Miaka ya nyuma nilikuwa nina aina mbili tu za Manukato.....moja ya Jioni (Organza) na nyingine ya kutwa nzima(Eden) harufu zake zinadumu muda mrefu....huitaji kujimwagia tena.


Nikaja kukutana na mdada mmoja anapenda Manukato kupita kiasi....kwamba akiwa na pesa ya ziada lazima anunue.....tena Designer ones.


Nikawa namshangaa nikisema anahitaji signature kwa maana aina moja au mbili tu za harufu basi nikawa namuita perfume addict.


Sasa leo hii napanga makorokocho yangu jikagundua nina Chupa kama Nane hivi za Manukato.....ama kweli hujafa hujaumbika!


Kati ya hizo zote my classicO Organza haipo sababu iliniudhi nilipokuwa mjamzito kwa mara ya kwanza.....will have to revisit(kuinunua tena).....ila Eden made it!Unajua pale unapendezwa na Manukato ya Kiume sio harufu yake tu bali Chupa husika inapendeza ukiiweka pale kwenye dresser si eti?Basi unajifanya umemnunulia Asali wa Moyo kumbe kiukweli umejinunulia mwenyewe kwasababu huwezi kujipulizia Manukato ya kiume basi unamnusa yeye.Well sinywi Pombe wala kuvuta Sigara......najipulizia Perfume kila siku na harufu yale.....hakuna siginecha hapa!

Babai.

Monday, 23 March 2015

Best Umri wa kufurahia Maisha.

Habari yako?

Je kuna umri uliopita na ukadhani ulifaidi sana na kufurahia maisha kuliko sasa au miaka michache kati kabla ya umri ulionao sasa?


Sijawahi kufanyiwa au kufanya sherehe ya siku ya Kuzaliwa sio tu kwa sababu za Kikacha kuwa hatuna hizi mambo (unaiga tu) lakini pia binafsi sipendi mikusanyiko ya watu na ikiwa naeza kuepuka kwa kutokuwa na Party basi na iwe hivyo....so yeah.
Naishi kwenye Nchi ambayo kutimiza miaka fulani ni big deal na hivyo mhusika kutaka ku-share siku yake maalum na watu wengine.
Hiyo ni Kacha yao na hivyo inawafanya (Kazini wanajua DoB na anuani yako so huna jinsi)baadhi wanipatie zawadi na hapo ndio suala la "am too old for the party ila zawadi napokea" linakuja  badala ya kuzikataa.Kuna umri ambao nahisi nilifurahia zaidi maisha yangu na hivyo kuzipenda namba au umri huo uliopita. Sikuwa chini ya Wazazi na sikuwa na majukumu. Nilifanya maamuzi bila kujali watu wengine....Baada ya hapo nikawa busy  na maisha.
Tangu Kibibi(princess) ameacha kunyonya full time nimeanza kufurahia Maisha tena, kwamba sasa nalala up to masaa 8!  Hakuna kuamka-amka mara kadhaa kila usiku.Naweza kumuacha na Baba yake jikaenda huko kwa masaa kadhaa bila kuhofia Matiti kujaa au Yeye kuwa na njaa......ni raha tupu!
Nimeisha kuwa wazi kuhusu suala la watu kupata hisia ya guilt kusema ukweli kuwa hawafurahii kuwa Mama(baada ya kuzaa).
Kama unalala masaa 4 ya kukatisha na upo on the go na wanao wawili chini ya miaka 5 na unafurahia Maisha yako basi wewe ni vere vere spesho au sio wa Dunia hii.

Babai.

Sunday, 22 March 2015

Mwanao anapoleta the Ex Factor


Kwa wale ambao Uhusiano wa bf na gf uliharibika na kuvunjika kwa sababu zozote na kwa bahati mbaya mlizaa (ukizaa na mtu halafu ni X mwenzangu ni bahati mbaya).


Sasa imagine kila unapowakorofisha watoto......watoto hukasirika tu hata kwa yale mema kwao.....mf unawakataza wasicheze Jikoni ni hatari au unahimiza wafanye home work badala ya kutazama Tv.


Kila unapokwenda kinyume na watakavyo kama mzazi kwa faida yao wanaanza kulia au kununa na kumtaja mama au baba yao......"Baba angekuwepo ingekuwa hivi au vile" au "mama angekuwepo asingenikataza hili au lile" na hiyo huwaongezea huzuni na hata kilia kwa Uchungu bila wewe kuwaona.Mara chache unaweza kusikia wakimtaja mzazi mwenzio ambae ni mama au baba yao lakini umeachana nae na sasa unamchukia.Nimesema hayo yote kutokana na tabia ya Babuu pale unapomuudhi(ukimkataza kufanya kitu).....ananuna halafu anasema "I want my dad to come and cheer me up".


Maneno hayo hunifanya nimuonee huruma (ndio atakacho) na kujisikia vibaya......halafu nawaza....Baba yake angekuwa Ex wangu.....yaani alinikimbia baada ya kushika Mimba aiiii mbona ningemkunyuga (chapa) huyu mtoto aisee. Well ningekasirika tu nisingempiga.Sasa wewe uliepo kwenye situation hiyo ya u-single baba/mama huwa unakabiliana vipi na hili? Huwa hupati mahasira kweli watoto au mtoto anapoleta the ex factor?


Usi panic mie nawaza tu kwa maandishi.

Babai.

Friday, 20 March 2015

Nakupa mapenzi alionipa Mama....


Unless hujui Elimu ya Viumbe Hai hasa kuhusu Mwanadamu utabisha na pengine kuwa offended.


Unaeza kudhani kuwa Ali Kiba amemkosea adabu Mama yake na pengine ulajiiliza utampaje mpenzi wako Mapenzi aliyokupa mama obviously hayato tosh......halafu ukawaza ni mapenzi gani hasa mwenzetu alipewa eeeh!Well uhusiano wa kwanza wa mtouo yeyote ni ule wa yeye na Wazazi wake.....mtoto hajui kupenda mtu yeyote zaidi ya wazazi wake hivyo lolote analopata kuyoka kwa wazazi hao ni mapenzi.


Linapokuja penzi la mama kwa mtoto wale wa Kiume au Baba kwa Binti yake kidogo kuna mkanganyiko na wengi hushindwa kuelewa lakini kama nilivyosema ikiwa kama unalijua vema Somo la Viumbe Hai baada ya High school(ambayo mie sikuipata hii ni another sitori ya siku ingine) utaelewa.


Vitendo vya kimapenzi au upendo ambavyo Mama alitupatia baada ya Kuzaliwa na kipindi tunakua ndivyo ambavyo tunavifanya au tunapenda kufanyiwa na Wapenzi wetu tukiwa watu wazima kwa......mf kunyonyana Chuchu, kukumbatiana, kupeana mabusu, kupapasana, hali ya kujali, kununuliana zawadi n.k.


Watoto nao hurudisha mapenzi hayo kwa wazazi wao.....well kwa mama tena zaidi kuliko Baba zao yaani mume husika. Hali hii hufanya baadho yetu kusahau kama kuna Mkibaba anauitaji affection pia.....sababu watoto wetu wanatupatia bila kusema kuomba yaani unamwagiwa  maafeksheni lundo daily kwa miaka ka 6 ya maisha ya mtoto bila "am not in mood" sababu ya stress za Kazi, ndugu, jamaa na marafiki.

Halafu mapenzi ya Mama hayaishi.....hayapungui wala kugubaa. Mapenzi ya mama ni ya milele hata kama mtakosana kibinaadamu (wakianza nataka mjukuu kabla sijafa .....simpendi mkeo).I wonder kwanini watoto wa kike huwa hatupewi nafasi ya kupata uzoefu wa mapenzi ya Baba zaidi ya kupewa kidole  unyonye pale unapomsumbua hihihihihi usiende huko mxsii lione!Anywaaaaaaay ukiachilia mbali kuwa napendezwa na Dogo (Ali Kiba) bado sioni kama amekosea kwenye Wimbo wa Chekecha.


Pamoja na kusema hivyo bado naelewa kwanini baadhi ya watu wanaeza kusema au kulalamika kuwa amekosea.Hey you sogea hapa nikunong'oneze......you need to go out a bit more.....hihihihihi natania!....namaanisha you need to educate yourself sio unapoteza Muda na Data kusoma Udaku tu ambao haukusaidii.Soma kuhusu Sayansi ya Viumbe na menhine ambayo unadhani kuwa huyajui au hukusoma ili kuepusha hali ya kuwa offended kichee.

Elimu kwenye Kiganja halafu hakuna Mtihani....how cool is that?

Babai

Thursday, 19 March 2015

Kuangalia na kujaji matako ya watu...!

Well sio watu wote bali Wanawake....halafu unacheka....i do!


Sidhani kama ni tatizo au tabia hii inanifanya nionekane Msagaji hihiiihihi.....(ngoja nijihami kabla hujaendelea kunijaji).....hapana sina hisia na wanawake wenzangu na wala siwatamani.Nikiwa natembea kwa miguu lazima nitakuwa naangalia makalio ya yeyote aliembele yangu na kulijaji tako lake halafu kama linachekesha basi nacheka.Tena matako ya Wazungu ndio yapo ya sampuli nyingi tofauti.....ujue sisi Waafrika(well Watanzania as sijawahi nzunguuka Bara zima la Afrika)...matako yetu ni ama yapo kwamba makubwa au ya wastani na yamejitokeza au hayapo yaani bapa.....hakuna ile eneo la tako kubwaa na bapa halafu kijitako kinajitokeza kiduchu kwa chini.


Au ni kwasababu Tanzania wengi hawavai Leggings sijui jeggins na viblauzi vifupi? Mmmh ukijifunga Khanga shape ya tako inaonekana so sidhani.

Hao ni wanawake. Linapokuja suala la Wanaume binafsi napendezwa na wanaume ambao ni Bapa. Mambo ya kukamata tako kubwa la mumeo nani anataka bana(napenda kamata kamata)......tatizo linakuja kwenye Kabila langu Wanaume wengi wana ma-hips(not really) wamejazia matokeo yake si ndio na mimi nikajipatia katako ka duara hihihihihihi.


Sasa pamoja na kuwa Wanawake wa Kizungu (wa hapa nilipo) wapo kama nilivyosema hapo juu bado Wanaume wao Mashallah(as in wana mawowowo yenye shepu njema)!Anyway.....Winter imeisha na imeniachia Cold na Mafua ya ajabu bana, nimeumwa Wiki nzima. Yaani leo ndio nimepata nguvu ya kukaa.

Babai.

Friday, 13 March 2015

MakeUps zinaharibu Ngozi ili uzitegemee?


Biashara ya Vipodozi inapamba faya mwaka hadi mwaka asante Beauty Gurus wa Youtube.....hata mie mpaka Mascara na lipgloss nimeanza kujipaka Foundation siku hizi(well nimeanza kupaka tangu 2004).

Enzi hizo mie napaka ilikuwa haiitwi Faundation bana, ilikuwa inaitwa cream to powder au mimi ndio nilikuwa sijui?hihihihihi.

The thing ni kwamba most Gurus (nakojifumzia kupaka make up) ngozi zao kama vile haziko sawa. Yaani kuna mmoja siku nilivyomuona bila make up (mambo ya GRWM as in get ready with me) nilaogopa kuendelea kuangalia.....sio kwamba anatisha la hasha! Niliogopa kusikitika na kulia (tangu mekuwa mama nimekuwa way too emotional).

Sasa ni mpango wa make up companies kuweka Viasili vya kuharibu Ngozi asilia ili uendelee kununua bidhaa zao na kuficha uharibifu uliopo Ngozini? Najiuliza.

Au ni kutokujua kwa baadhi ya watu na hivyo walikuwa hawasafishi Ngozi na kulala na makeups?

Pengine ni matumizi ya Vipodozi aka Makeup wakatu ngozi bado haijakomaa? Unajua kuwa Ngozi ni moja ya Ogani kama ilivyo Moyo na inakua kulingana na ukuaji wako...sidhani hii ilikuwepo kwenye Biology niliyosoma au kwa vile nilikuwa nasinzia(Mwalimu alikuwa so boring....akianza tu mie yuleee Kisarawe).

Au hali ya hewabya Baridi haipendi Ngozi nyeusi.....kwamba naturally inakinga ya kutosha kupigana na Jua sasa kama Jua halitoshi ngozi inasahau sijui masikini matokeo yake inapigana na Vipodozi(Doesnt even make sense I know).

Anyway.....kila biashara ina namna yake ya kuendelea....mf biashara ya software na Virus.....wanaotengeneza softwares ndio wanaotengeneza Virus ili biashara ya software iendelee kuwepo na wewe mtumiaji kuwa tegemezi.

Ngozi yangu inabadilika kulingana na hali ya hewa. Baridi napauka(a bit lighter)na wakati wa joto naiva(a bit darker).....lakini ile cream to powder haikunibadilisha....kwanza hata nilipaka Foundation hujui.


Ama sijui kujipaka au kwa ujumla sirembeki hihihihi sura gumu mpaka Make ups zinadunda.Napenda makeup sababu inanipa kale ka muda ka mimi kuwa peke yangu bila adha ya watoto na baba yao. Ila hiyo issue ya Ngozi kuwa mbaya ndio inanikatisha tamaa.

Leo ni siku ya Mikosi UK.....kila Ijumaa 13. Happy 1st Mikosi day of 2015.

Babai.

Thursday, 12 March 2015

Kupenda watoto wa watu.


Mawifi na marafiki wa Kike wa mumeo ndio viongozi wa kujifanya wanapenda watoto wa watu.


Utasikia "aah jamani waambie nawapenda sana"......mie najibu kimoyo-moyo, unauhakika unawapenda wanangu? Ukikaa nao wiki tu utabadilisha mawazo.....they are hard work!Mimi ni Wifi na Shemeji pia lakini sijawahi kusema nawapenda Wapwa zangu.....ninahisia nao nafurahi kuwaona na kuongea nao lakini siwezi kusema nawapenda wakati sijawahi kuishi nao.


Uwazi wangu kuhusu hisia za kupenda watoto wa watu hufanya baadhi ya watu kusema kuwa nina roho mbaya kwamba nachukia watoto.


Mie sijui kudanganya kuwa nawapenda wanao wakati najua wazi moyoni hawapo. Nachukulia watoto wote kama watoto na sipendi waonewe au wateseke na hilo ni muhimu zaidi kwangu kuliko kukudanganya kuwa nawapenda.


Kwasababu tu ni mtoto haikufanyi automatically umpende.....nilikuambia kwenye moja yabpost zangu, baada ya kuzaa wanangu sikupata ile hisia ya kuanguka kimapenzi kwa mara ya pili na ya tatu baada ya Baba yao kama wengi wanavyodai.


Kuna possibly hakuna hisia kama hiyo ila ni mchanganyiko wa furaha ya kumuona mwanao baada ya maumivu ya Uchungu na  ile hali ya wuhuuu it is over!!

Kingine ni guilt (mawifi wanqkughukia ili kuficha hilo kwa kaka yao wanakimbilia nawapenda sana wapwa zangu) au kutaka kuwa karibu na Baba yao.


....hihihihihi unawajua wale wa "jamani watoto wazuri, nawapenda natamani wangekuwa wangu".....hawa husema hivyo kwenye profile ya mumeo tu sio yako.

Eeh Babuu si katimiza miaka 4.....asubuhi yake sasa kaanza "mum is today my birthday".....nikasema ndio....babuu:yay...mum you forgot to say something.....nikasema nini? Babuu: sing happy birthday song.

Umegundua nini?

Kaniita mum na sio mummy kama kawaida ya watoto chini ya miaka 6. Aah my boy is a grown man.....sort of.

Babai.

Tuesday, 10 March 2015

Malezi kwa Culture ya Ughaibuni....


Ni kawaida kwa baadhi ya watu(nilikuwa mmoja wao) kushangaa na kuwashutumu Wazazi wa kitanzania waishio Ughaibuni kuwa "wanaiga" na wanalea watoto wao "kizungu" na kusahau au kutojali Kacha yao.


Unapomzaa mtoto London kwa mfano na mtoto huyo kuendelea kuishi huko maisha yake yote unategemea mtoto huyo atakuwa na Kacha ya kwenu?Mazingira, Vyakula na Mtindo wa maisha ya wanajamii yanauo mzunguuka ni ya Kacha  ya Nchi husika alikozaliwa na anakulia hivyo sio sahihi "kumpinda" afuate Kacha yako wakati yupo kwenye mazingira tofauti na yale uliyokulia wewe huko kwenu ulikotoka.

Mtoto husika anakuja Tanzania mara moja kwa Mwaka na kukaa huko kwa wiki 2-3 na unategemea akue kama wewe na kufuata kacha yako?


Ni vema na muhimu kuendeleza values zako na kuwaeleza watoto tofauti ya Kacha yako na Kacha yao lakiji sio kuwalea Kisarawe wakati wanaishi Kent.


Just because wamezaliwa na Mtanzania na wao wanautanzania sio lazima wafuate Kacha ya Kitanzania.


Jinsi wanavyokuwa na bidii yako ya kuwaelisha kuhusu asili yao, Historia ya Nchi yako TANZANIA na Utamaduni wenu ndivyo itakavyowasaidia na pengine kuamua kuishi KisaraweAN au Kibritain.


Mbona nyie hamuishi Ughaibuni na baadhi hamjawahi kufika lakini mnalea wanawenu kiughaihuni bila hata kuwa na Mazingira ya Kiughaibuni?

Mtuache.

Babai.

Wednesday, 4 March 2015

Stop....Africa is NOT a Country.

Mtukome......

Wamarekani ndio zao....sijui hawakuwa na waalimu wa Jiografia. Wakija UK wanasema wanakuja EU.....wakienda Tanzania wanasema wapo Afrika.

Mbona Canada hamuirifai kama America au Marekani ya Kaskazini?


Humkuti mtu kutoka Bara la Ulaya anarifaa Nchi yake kama Ulaya....atakuambia moja kwa moja yeye anatoka wapi.


Afrika ni Bara sio Nchi. Halafu waafrika wenyewe ndio mamwehu kabisa yanaona raha au sijui sifa au aibu ku reffer Nchi zao walikotoka na kuishia kusema Afrika....."back home in Africa nlanlanlaaaa".


Sema Nchi yako kama hawaijui waambie wakaGUGE......acheni kutufanya as if Waafrika wote tupo sawa.Nchi yeyote iliyotawaliwa na Muingereza inafuata mambo fulani ya Kiingereza.....kuna Tamaduni tume-adopt na kufanya zetu....mfano Ukristo, uvaaji wa nguo na baadhi ya Uendeshaji wa shughuli za Kimahakama bila kusahau sheria. Hii ndio faida pekee ya Jumuiya ya Madola(in my head).


Halikadhalika waliotawaliwa na Mreno....Mwarabu....Mjerumani au Mfaransa wanafuata Tamaduni za Nchi Tawala.


Pamoja na kuwa tuna baadhi ya vyakula sawa....utagundua upikaji na Ulaji wetu unatofautiana.


Pia maumbile yetu ni tofauti....tabia zetu ni tofauti....uchangamfu na wepesi  wa akili na utendaji ni tofauti.


Wenyewe tu ndani ya Tanzania tumetofautiana depends na Kabila....Mf Wapemba na Wachaga wazuri sana kwenye Biashara kuliko wale wa Kagera  ambao ni wazuri kwenye Kitabu na majivuno.


Tabora wapo vizuri kwenye nanilihu....Academically lakini wavivu kimaendeleo.....majungu....misifa na wanapenda kukimbia Mkoa wao (wahamiaji wazuri) kuliko Wazaramo ambao sio wazuri sana Academically lakini wazuri kwenye suala la kuendeleza ardhi.....Mzaramo bana kumiliki Kibanda ni muhimu. Umewahi sikia msemo kuwa "mzaramo halali njaa"?


Wale wa Sinza (is Mkoa now au)ama wanalelewa na KugaZ au ni Vimada (hihihihihi)....no offence intended.....niliipata hii nilipokuwa Morogoro(siku nikikumbuka ntashea).


Sasa ikiwa ndani ya Tanzania tunatofautiana mpaka Desturi iweje muirifae Afrika kama nchi wakati tunatofautiana kidesturi n.k?

Kesho basi au vipi?

Tuesday, 3 March 2015

Kwanini___haonyeshi mtoto wake?

Hujawahi kujiuliza kwanini huyu fulani anapenda kuzungumzia mwanae lakini hajawahi kuweka picha ili na mimi angalau nipate picha ya alivyo kila anapomzungumzia.


Well shauri yako ila najua mie nimeisha jiuliza to the point napata hasira(hihihihi sio hasira bali whys lundo).

Kuna dada mmoja (enzi zile bado nipo kwenye social media) alikuwa ana-share mengi wakati wa Mimba....alimalizia na baby shower na habari ya mtoto kuzaliwa halafu ndio ukawa mwisho.....akawa anamzungumzia tu na kushare zawadi alizompatia kwenye Siku ya kuzaliwa n.k....mapaka leo sijui sura wala rangi ya mwanae......sio muhimu kihivyo lakini muhimu.

So kama mimi enzi nilikuwa nahisi hivyo hakika hata wewe ungependa kuona sura za wananhu si eti eeeh.


Nili-share picha kiasi nilipokuwa kwenye Sosho media so walionifuata wengi wanakumbukumbu kwa mbali ya wanangu walivyo japo sasa wamekua mmno.

Kuna sababu nyingi zinazofanya watu kuzuia picha za watoto wao kuzagaa mitandaoni hasa kama wazazi ni maCeleb.....

.....maana hakuna mzazi anataka kuona comment mbaya kuhusu mwanae hata kama ni za kweli.....au wengine wanahamishia chuki zao kutoka kwa Baba Celeb kwenda kwa mtoto....so unfair.

Kwa sisi wa Ulayani ni tofauti kidogo.....ukishare nyingi unaweza anza kufuatiliwa kwanini wa-share kila pic....mpaka za mtoto anaoga au kujisaidia....unaeza nyang'anywa mwanao kwasababu ya kupitiliza kushea mapicha ya innocent tots bila idhini yao watoto.


Halafu wanapokuwa shule unakamatwa na Policy....kila Shule ina policy yake sasa ikiwa mtoto anasoma Shule ambayo hawataki uweke picha za mtoto Mtandaoni ili kuepuka bulling na misuse sasa au huko mbeleni.....kidogo inakuwa ngumu.


GOOGLE na Tecknology imefanya Dunia kuwa Kijiji.....mtu anaeza kumfuatilia mwanao kwa picha unazoweka na ile kafikisha miaka kadhaa tu anamdaka na uyhibitosho wa Picha zote za utotoni mpaka hapo alipo.


Enzi nasoma Msingi kuna msichana alimkana Mama yake.....kwa vile tulikuwa hatumjui ilikuwa rahisi kumuakini....sasa watoto wa leo watatukana vipi hasa kama Wazazi wenyewe wapuuzi puuzi na habari zetu(sio mimi bana  wao khaaa....mie ananijua nani) zimejaa online.


Something like....your dad cheated on his wife with your mum for you to get life(sababu ya wewe kuwepo Duniani was a dirty nanilinhu).....si unawajua funs bana.

Babai.