Tuesday, 16 February 2016

Kujua kila Kitu vs Kujua kila situation ya Watu........nirahisi kupatwa/kabiliana  na mengi kwenye Maisha yako na hivyo kujifunza zaidi, kuliko kujua kila situation ya mtu, achilia mbali watu ambao sio wewe. Niliwahi ku-blog kuhusu tabia ya watu "kujifanya" wanamjua kila mtu au zaidi "celeb" na life situations zao. Hakika hilo linawezekana, lakini ni vema kuweka wazi kuwa unayajua hayo yote kwasababu ya kusoma Gossip Sites/Blogs/TvChanells/Vijiwe/Joints n.k. na sio kwamba unawajua hao watu individually.
Kutokana na Maendeleo ya Kiteknolojia,  mawasiliano yamerahisishwa na hivyo baadhi yetu huwa tunapata Majibu/Ushauri wa Maswali/Matatizo yanayotukabili papo kwa hapo. Urahisi huu unafanya wengine kupitiliza kwenye kuchangia "uzoefu" wao kwenye "situations" nyingi kwenye Sosho midia husika na hivyo kukera baadhi.

Mie binafsi nina majibu mengi zaidi kuliko your "normal" Dada, kwasababu pengine n iliyopitia mimi kwenye maisha yangu na kujifunza au kupambana na kutatu ni tofauti na Dada yako au Pengine Wazazi wako ukiwachanganya pamoja(hihihihi this sounds ka' tusi) na  hata Mwalimu wako! Najua Mengi Kimaisha lakini sijui Kila kitu.
Hivyo huwa sishangai au kumkejeli yeyote ambae anaushauri/jibu kwenye kila jambo au mambo mengi(wewe huamini kuwa mtu huyu mmoja anaweza kupitia yote hayo maishani). Kuna Magonjwa mtu  amekabiliana nayo, ambayo watu wako hawajawahi kuugua. Kuna changamoto nyingi tofauti alizopambana nazo katika maisha yake nakushinda wewe hutokaa uzipate, Huenda anafanya kazi kwenye jamii na hivyo anakutana na Mengi anapokuwa kazini na hivyo kujifunza even more!
Sio hayo niliyoyataja tu bali kuna mengine anashuhudia na kuhusishwa na ndugu/jamaa zake ambao wanapatwa na matatizo ya Dunia, na yeye akajifunza, sasa badala ya kumsimanga/mcheka/kejeli mtu kuwa "anajifanya" anajua kila kitu au kumshangaa "haiwezekani ajue kila kitu" kumbuka na zingatia hili  Mwalimu Bora  Duniani ni Uzoefu wako Binafsi pia Mengi sio Yote!Ahsante kwa muda wako hapa, Nathamini na kuheshimu uamuzi wako wa kuichagua Blog hii.

Babai.

Monday, 15 February 2016

Mtoto "anaechagua" Vyakula....

....ndio mnaita "Fussy eater" eti?

Baadhi ya Watoto huanza mapema(au wazazi wao wanaamua kuwa watoto wao ni fussy kama sifa) katika hali halisi ni Uchovu unaopelekea kutokuwa na utararibu wa "kula" na attention ya kutosha kwenye kula kwa mtoto husika!


Kamwe sitokufunza namna ya kule mwanao, isipokuwa nitachangia uzoefu wangu ili kwa namna moja ujione kuwa haupo peke yako na hivyo kupata nafuu na pengine kuchukua "tips" na kujaribu ili mwanao apate virutubisho vyote Asilia ambavyo ni Muhimu kwa Ukuaji wake.Mwanangu wa Kwanza(Babuu) alianza kula Vizuri sana akiwa na Miezi Sita, alipofikisha Mwaka na Miezi 3(Miezi 15) akacha kunyonya mwenyewe(bila kuachishwa). Babuu alikuwa anakula kila aina ya Chakula unachompatia. Alipofikisha Miaka 2 hali ikabadilika, akaanza kukataa Nyama na Samaki which was Okay kwasababu alikuwa akila Mayai vema. Alipofika Miaka 2 na Nusu akawa anakula Viazi tu.....tena viwe vimepondwa(mashed).
Ukichanganya Mchuzi au Mboga-mboga kwenye  Viazi vyake "mashed", anasema "sipendi harufu" so anagoma kula na kuomba Maziwa.....then unampa Maziwa wakati anasubiri umtengenezee Viazi vingine bila "shombo". Mimi kama mimi, nikabeba Mwanangu huyoo mpaka kwa Daktari wake nakushtaki(kuelezea), Daktari akasema so long anakula Viazi, Mayai na Maziwa ni okay, ila niongeze matunda between meals! Hapana, sikufanikiwa.....tukarudi na kubaki kwenye  Viazi vya kuponda/Saga.
Wataalamu wanasema kuwa ni kawaida kwa Mtoto kuwa mchaguzi linapokuja suala la kula na kwamba ni sehemu ya Ukuaji. Wao wanatoa "Tips" kwa ujumla ili wazazi wenye watoto fussy tuzijaribu....napenda kukuhakikishia kuwa  nimejaribu zote na hakuna hata  moja iliyonisaidia.
Nikagundua kuwa Mama (au anaekutunzia mwanao unapokuwa Kazini) unakuwa na shughuli nyingi na zile Homono huwa hazijirudi haraka kwa baadhi yetu na hivyo kuna wakati unajisahau na badala ya kumpa mtoto chakula unampa maziwa kwanza ili aponze  njaa kisha ndio chakula(hapa lazma akatae), kosa ni kuwa anaponyonya njaa inakwisha, watoto sio kama sisi watu wazima. Kwamba njaa ikuma unakunywa Chai na kipande cha Mkate wakati unasubiri chakula kiive, Maziwa tumboni mwa mtoto wa umri wa Miezi 6 hadi miaka 4  hudumu kwa Masaa2+.Kumbuka, mtoto bado anajifunza kil akitu kwa mara ya kwanza, sasa usipokuwa na utaratibu unaojirudia utakaomfanya azoee na kuona kuwa ni "kawaida" anachanganyikiwa na kusahau at the same time!Sasa ile kutokuwa na utaratibu unamchanganya mtoto (kama nilivyosema)na matokeo yake anaanza kuchukia kula(unamlazimisha kula wakati hana njaa), hii haina "mtoto anataka kujitegemea kama Wazungu wanavyosema", hii  ni Mzazi/Mlezi kutokuwa  na utaratibu unaojirudia na wao kula kama Mazoea badala ya kula ili wapate nguvu/wakue(nia ni moja kuwa wale wakue na kujenga mwili ktk mtindo tofauti).Haikuwa kazi rahisi kumfanya Babuu aanze kula vizuri au niseme kawaida (isipokuwa Nyama), Zifuatazo ni Tips zangu Binafsi ambazo zinaweza kukusaidia  kama Mwanao ni Fussy eater;-


easy way kupata Matunda na Mboga 5 a day

1-Weka utaratibu wa Masaa ya Kula, Mf: Saa 8 Kifungua kinywa, Saa Nne na Nusu Snack, Saa Sita  Mlo wa Mchana , Saa nane na Nusu Snack, na Saa Kumi  na Moja Mlo wa Jioni na Saa Moja jioni Maziwa(husisia ku-relax na hivyo analala haraka)2-Usizidishe kipimo kwenye "snacks", kumbuka hii ni kupitisha muda kabla ya Chakula, sasa kama umeweka Maziwa/mayai ndio snack basi hakikisha unampatia kidogo ili asishibe.3-Mpe Choice(kama uchumi unaruhusu na anamika 2+), Utapenda maziwa na vitumbua au Maziwa na Mayai?....anaweza kusema Mziwa tu, mwambie ale kitafunwa kwanza halafu atapata Maziwa.4-Usimfokee, usimkaripie na wala usimlazimishe kula.....mbembeleze kula, ikiwezekana Mlishe(memlisha Babuu mpaka mwaka jana hihihihihi).....achana na  ile "tukienda kwa watu itakuwa aibu mtoto wa miaka 4 bado namlisha",...pima Wao vs Afya ya Mwanao.5-Kama kuna shughuli, hakikisha unambebea mwanao chakula chake unachojua anakipenda, ikiwezekana mlishe kabisa kabla hamjatoka.
6-Chagua aina moja ya Mboga ambayo ni "super food" lakini haina Harufu/Radha kali.....mie nilichagua Mchicha na Kale. Changanya Tutunda tamu na laini kama vile Papai, Embe, Zazibu, Ndizi na Moja ya Mboga hizo zikiwa Mbichi(bila shaka ni baada ya kuosha ) halafu changanya Vijiko Viwili Vikubwa cha chakula kwenye Mlo wake wa Mchana au Jioni. Na ikiwa mwanao ni mpenzi wa Mash basi ni nafuu kwako na kwake.
Kumbuka Mwanao ni  tofauti na hakuna kama yeye Duniani, ni an individual/his/her own little person hivyo usimfananishe/linganishe na watoto wengine wa umri wake au wadogo kwake. Muhimu ni kwa Mwanao kupata uzoefu wa radha tofauti tena kama ilivyokuwa mwanzo wakati unaanza kumtambulisha kwenye vyakula ili aache kunyonya, tofauti sasa  ni Mkubwa na anahitaji virutubisho zaidi kwani havipati via Nyoyo yako anymore. Amekuwa so Mashed kila kitu ni muokozi wako kwa sasa.Inakatisha tamaa, inachosha wakati mwingine.....lakini usikate tamaa. Jaribu Tips zangu.....hata akila vijiko 3 bado mchanganyiko huo utamsaidia ndani na nje ya Mwili.


Babai.

Friday, 5 February 2016

Mzazi Mkali Vs Mpole....


Hello!

Utakoma na Post za Wazazi na Watoto mahali hapa, ni maisha niishiyo sasa na sio mbaya kama nikichangia uzoefu wangu ambao pengine unafanana na wako na hivyo kukufanya kujisikia nafuu kuwa haupo peke yako au ukanishangaa. Vilevile inawezekana kabisa ukajifunza jambo!
Hofu yangu kuu ni Waanangu kuwa na Tabia mbaya chini ya uangalizi wangu, kutokuwa na Heshima kwetu Wazazi wao na Watu wengine. Hofu hii ndio iliyochangia mimi kujitolea Mhanga na kuwa Mama wa nyumbani kwa Miaka 3.  Sikutaka Wanangu waje na tabia za "Nursery assistant".....Babuu alianza Nursery akiwa Mchanga as bado nilikuwa na ile " I can do all, independent woman".....untill Mwanangu alipoanza kunikataa na kulia kwa Uchungu kila nilipokuwa naenda kumchukua!
Vilevile alipofikisha Miezi 8 akawa na "vijitabia" ambavyo siku pendezwa navyo.....Solution? nikapunguza Masaa ya Kazi na Nursery(so kutoka full time akawa anaenda kwa 5hrs). Niliamini(bado naamini) kuwa Mtoto anahitaji Mama yake  24/5 (ondoa  Masaa ya Nursery) Miaka 5 ya mwanzo ya Maisha yake(mie sio Feminist so nisamehe kama sitomtaja sana Baba).
Kiasilia Mimi ni Mkali(sipendi ujinga), inawezekana ni kwasababu ya kuwa na wadogo wengi zaidi kuliko kuwa na wakubwa(mie ni wa Pili kuzaliwa na ni Dada mkubwa). Ukali wangu ni kwa watoto wote sio wadogo zangu tu(walipokuwa wadogo) bali hata kwa watoto wa Watu niliokua na "babysit" au wale waliokuwa wakija kunitembelea kutokana na kufahamianakwangu na Wazazi wao.
Pamoja na Ukali pia mimi ni Manners "fanatic"(usiende kuGugo), nachukia watu/watoto wasio na Manners. Mara zote huwa napitisha Hukumu kuwa Mama zao hawakuwafunza, kwasababu naamini mtoto anajifunza "manners" kati ya Miaka 2 na 5, uki-"lemaa" katika Umri huo basi wewe na wao are done!Kuanza kumfunza mtoto Manners katika Umri mkubwa ni kazi zaidi kuliko umri nilioutaja hapo juu, umri wa Miaka 2-5 mtoto hujifunnza "misingi" ya mambo mengi na kuitunza, hivyo ukianza  mapema inakuwa rahisi "kumkumbushia" akivuka umri huo kuliko kuanza upya.
Kumbuka mtoto anapozaliwa huwa hajui kitu(well labda kunyonya), Ubongo wake huwa "pure", sasa yote mfanyayo kama wazazi au Mlezi(kwa wale wanaoachia watoto watu wengine) huwa ni mara ya Kwanza kwa Mtoto. Mungu anisaidie na kunipa nguvu ili Wanangu wakue wakijua umuhimu wa kuwa Wema, kuheshimu, kuomba na kushukuru.
Kwenye Familia yetu ya watu Wanne, Mimi Mama ni Mkali/Mnoko) na Baba yao ni Mpole(laid back)....kuna mahali tulikuwa tunapishana kwenye malezi, kwamba mimi nikikataza Watoto wasifanye jambo, wanakimbilia kwa Asali wa Moyo(baba yao) na yeye anawakubalia. Ikafikia Dad akawa their best friend na mie nikawa sio Friend of any sort hihihihi.Ikabidi "Work as a Team" iingizwe ili Watoto wajue kuwa Mama akisema HAPANA basi hata wakikimbilia kwa Baba ni HAPANA. Haikuwa rahisi kama kwenye  kila kitu  unachowafunza kwenye Umri huo mdogo.


Pamoja na ukali wangu, sijawahi kuwachapa, vitisho kama "I will call Nunda for you", "will give you Time out", will taka away Toys au Tablets bado zinafanya kazi. Sasa wewe ni Mzazi wa aina gani/ Mkali/Mnoko au Mpole?


**Nunda= to them is like a Monster


Ahsante kwa Muda wako hapa, nathamini na kuheshimu uamuzi wako wa Kuichagua Blog hii.

Babai.