Monday, 6 August 2018

Kama Mumeo anakupenda hatoruhusu ufanye haya...


Kutokana na wakati tuliopo ambapo  kuna "informations" nyingi kuhusu nini hasa Mwanamke anapaswa kufanya au kuwa na hivyo kuibua kukanganyana na kudanganyana kuliko wakati wowote ule wa maisha ya Mwanadamu(nimeongeza chumvi, sijui historia ya Mwanamke kabla ya 1900). Hata hivyo bado haiondoi  ukweli kuwa kuwa Mwanamke  mbele ya Wanawake wa kisasa ni Kazi ya Ziada.Mara nyingi sie(wewe na wenzio) wa Kisasa huwa tunaambiana kuwa mwanaume hana haki juu ya mwili wako au uamuzi wako wa nini unataka kufanya na mwili wako(mavazi/Urembo) which it is true  kama ni Mpitaji(boyfriend) lakini ukiwa  kwenye Ndoa/Uhusiano Mwanaume kuonyesha kuwa anajali nini unaweka juu ya mwili wako ni dalili kuwa mwanaume huyo anakupenda na sio kwamba hajiamini au anahofua kuibiwa.Wengi mnadanganyana kuwa Mume(au Mume mtarajiwa) akikukataza usifanye mambo kadhaa ni kuwa anaku-control, Nyanyasa au ni Dikteta kwenye uhusiano wenu. Tunasahau kuwa yeye ni mwanaume na hivyo anajua ni namna gani Wanaume wanavyotuona, wanavyotuchukulia tofauti na sisi wanawake tunavyojiona/chukulia.


Mwenza wako anakupenda ikiwa haruhusu yafuatayo;-

*Utoke peke yako(au na Watoto kama mnao) ukiwa umevaa nguo fupi/zinazoonyesha baadhi ya maeneo ya mwili wako ambayo yanavutia. Ukibisha/lalamika ooh "ulinikuta nikivaa hivi na ukanipenda, niache usinibadilishe". Atakubali na atasisitiza uvae hivyo ukiwa nae au ukiwa nyumbani.

Yeye kuweka zuio hilo sio kwamba hajiamini  kama unavyodhani bali ni kujali usalama wako  na kuepusha adha ya Wanaume wengine kukukosea/shushia heshima(miluzi, kutoa maneno ya kukutamani au kukufuata/shika).


*Ulale usiku mzima ukiwa na hasira, hata kama umewahi kulala kabla yake atahakikisha anakuweka karibu ili ujihisi "protected", sio mara zote ukiamka mikononi mwake baada ya kukasirika ni kwamba anataka Ngono. Wakati mwingineni kuomba msamaha na wakati mwingine ni kukulinda au vyote.


*Kupoteza mvyuto wako, hatokwenda kulalamika kwa watu kuwa umekuwa mchafu au hujipendi tena tangu umejifungua watoto wenu bali atakukumbusha mf; "Mke wangu enzi ulikuwa unajipenda sana, ulikuwa hutoki nje bila kujiremba, namtaka mke wangu yule wa enzi" na atakusaidia kukabiliana na majukumu ya nyumbani na mtoto ili upate muda wa kujijali na kujirudishia mvuto wako tena au zaidi ya ulivyokuwa kabla ya Mtoto kuzaliwa.


*Ujishushe, mf; Ki-career au kimuonekano. Ukilalamika kuwa umekuwa sio "smart" tena na pengine umekuwa sio "ambitious"  tena labda ya kukaa nyumbani muda mrefu(Likizo ya Uzazi), yeye atakupa wazo la ama kubadili career(rudi shule), kamwe hatokuambia "natengeneza pesa za kutosha, au nitaongeza huitaji kurudi kazini". Ukiamua kuwa mama wa nyumbani itakuwa ni wewe binafsi.


Ukilalamika kuwa umenenepa/konda nakupoteza shape  na hupendi ulivyo...kamwe hatokuambia "fanya mazoezi upungue au "kula unenepe" atakuambia na  kukuhakikishia kwamba yeye haoni tofauti na uache upuuzi(kujishusha).


Ukisisitiza sana(labda kwa vile kweli unajisikia ovyo sababu hujazoea mabadiliko ya mwili wako) basi atasema "kama ni muhimu kwako  basi kupungua/nenepa ila kwangu you look sexier after kids"..


*Mtu yeyote kukushushia Heshima hata kama ni Mama yake, achiliambali ndugu na marafiki. Pengine anaweza asioneshe hivyo moja kwa moja lakini mara zote atakuwa upande wako na kujaribu kukulinda na kukuondoa sehemu ya tukio. Ata-deal na watu wake na kuwaonya kuwa hataki kuona wanakushushia heshima.


Mumeo anaku-control, Nyanyasa au ni Dikteta ikiwa tu;-

Aanakukataza usiwe na marafiki(wazuri), usitembelee Ndugu, Usiunguze chakula hata kwa bahati mbaya, anakupiga, anakutukana, hakuheshimu mbele ya Ndugu zake, hafanyi mapenzi na wewe(anafanya ngono tu), hataki ujitegemee Kiuchumi, hajali career yako n.k.Ahsante kwa kuichagua Blog hii, tambua kuwa nathamini muda wako hapa.
Bai.