Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2021

Kujali(nguzo 5 za Mahusiano.

 Huwezi kuwa Mke bora ikiwa hufanyi mambo Milioni moja na nusu ikiwa ni pamoja na Kujali.  Kujali kwenye Ndoa  sio kitu kinachotakiwa kufanywa na Mke, bali Mume pia. Japokuwa  kwenye jamii Mke ndio hutegemewa kuonyesha kujali zaidi kuliko mwenza wake wa kiume. Mke atahakikisha Mume analala mahali safi na comfortable, nyumba safi na inapendeza, Nguo na hata Chakula kimeandaliwa vema na kwa wakati. Mke hatoishia hapo, atajiswafi na kujiremba/pendezesha/nukia vizuri kwa ajili ya Macho na Heshima kwa Mume(watu watakao kuona nje). Mke ataendelea kutoa ushari, kumtuliza, kumpa moyo/matumaini, kum-support, kuhakikisha ana Afya njema na kumkumbusha suala zima la kuilinda Afya yake. Ikiwa mnaishi mbali na Wazazi wa Mume, Mke atakumbusha kuwajulia hali na pengine kwenda kama Familia ili wasipoteze ukaribu kwako na Wajukuu zao. Mwisho kabisa, Mke atahakikisha watoto wanakubuka siku Muhimu kwa Baba yao na kukupatia vijizawadi kwa niaba yao(Watoto)   Uliza Mumeo anakujali kwa  kufanya nini? Kwa 99%