Skip to main content

Posts

Uelewa na kumbukumbu ya Mtoto.

Nilipotobolewa Masikio nilikuwa na Miezi Sita (kwa Mujibu wa Mama), alienitoboa ni Mama wa Kimasai na aliekuwa kanibeba/shika ni Bibi yake Mama. Sikumbuki maumivu, lakini nakumbuka nililia sana nilipomuona Mama wa Kimasai na Shanga zake na Masikio yakiwa marefu "kwenda chini". Siku niliyomsimulia Mama kuhusu hiyo siku ya tukio (nilikuwa teen na bado naikumbuka)...alinishangaa na kusema kuwa lazima nilisikia akisimulia watu, mtoto wa miezi Sita hawezi kukumbuka. Nilipokuwa na miaka 3 au zaidi, tulikuwa Mjini Mbeya....Mama, Mimi, Mjomba na watu wengine tulikuwa tunapita pembezoni mwa Mto. Mjomba wangu alinibeba na kutishia kunirusha kwenye Maji(Mto)....Nadhani ndio maana naogopa Maji....Safari zangu ni za Anga, Reli na Barabara, mie Meli sijui Boti sipandi....Mtumbwi? Bora uniue. The point is, Mtoto anauwezo wa kutunza kumbukumbu kuanzia umri mdogo sana kuliko tunavyoaminishwa na "Mzungu" the Shenzi. Sio unafanya mambo u

Kaja for a reason....

Wacha kujipa Moyo.....hakuna mtu anajiijia tu maishani mwako isipokuwa wewe unaruhusu awe/aingie Maishani mwako. Ukisema umefanya maamuzi mabaya ya kuruhusu huyo particular mtu maishani mwako nitakuelewa. Kumbuka wewe ndio responsible kwa kila kinachotokea maishani mwako iwe ni maamuzi mazuri au mabaya.....beba mzigo na ujipange upya, sio kujipa-jipa moyo...eti sababu Mzungu anakuaminisha kuwa "people come in your life for a reason". Kuna watu wanaishi ili kuharibu maisha ya watu, ndio furaha yao. Wengine walikosa mapenzi na malezi bora kutoka kwa Wazazi/Walezi matokeo yake wanayatafuta waliyoyakosa kwa kuharibu maisha ya wenzao.....nakadhalika. Sasa ni juu yako kumsoma yeyote anaekuja maishani mwako na kumruhusu aingine kama Rafiki, Mpenzi, Jamaa ( wale mliooa/olewa Ukoo Mmoja), ukigundua tu kuwa umekosea basi haraka muepuke kabla hajaharibu zaidi. Nikupe mfano?....I looooooooooove mifano hihihihihi(watu tunauelewa tofauti, bila mifano wengine tunatoka kapa). Unaishi maisha

Mali ya Familia...

Kuna baadhi yetu tunatabia/kasumba ya kuita Mali za watu kuwa zetu na pengine kuanzisha fujo na kupelekea Vita kubwa ili kila mmoja apate "mgao" wake. Kwasababu tu Mali ni za Baba/Mama yako au Kaka/Dada yako haikupi haki ya wewe kupata Mgao....wacha papara za kutaka kunijibu, nitakupa mfano ili unielewe vema. Baba na Mama wameachana wakiwa hawana kitu, Baba kaanzisha uhusiano mwingine na kupata familia "mpya"....mambo yakaenda vema wakawa na Mali za kutosha....wewe uliezaliwa na Mama wa kwanza unadhani una unahaki na Mgao sawa kama watoto waliomo kwenye "familia Mpya"? Upatikanaji wa Mali za Baba yako na familia yake Mpya unamchango Mkubwa wa Mama yao (familia Mpya) na sio Mama yako (alieachana na Baba yako akiwa hana kitu)....sehemu ya mali utakayoipata ni ndogo sana, tena kama Mke atakubali upatiwe. Mf; wa kwanza. Mf wa Pili: Dada/Kaka kajipinda na kujituma yeye na Mume/Mkewe na sasa wanamiliki Mali nzito, inakuaje wakubwa/wadogo watu mhesabu kuwa hizo