Skip to main content

Posts

Umewahi ombwa Mchango wa Birthday?

Huu ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa heshima wa Vipato vya watu....hii kwa Michango yote isipokuwa Ada ya Shule. Kama humudu kulisha watu kwenye sherehe ya kuadhimisha siku yako ya kuzaliwa si uachane na issue nzima ya Sherehe!! Kujitegemea Kiuchumi kumegawanyika katika makundi mbali mbali ujue...(sina uhakika, najaribu kulazimisha tu hapa hihihihihi).....! Kuna baadhi ya watu ambao huishi kutegemea wenzao ili kufanikisha mambo au jambo kwa faida zao Binafsi......wandugu jitegemeeni kiuchumi EBO!!! Mchango wa Harusi: Wakati harusi(Bikira) yenyewe wewe na mtarajiwa wako hamna hiyo HARUSI. Kama hamuwezi kulisha wageni wenu kwa kutumia vipato venu basi fungeni Ndoa mkiwa peke yenu wawili na mashahidi....eti? Siiiiiiimple + no stress. Birthday Party: hii sinimeisha isema kule juu? Eeeh kuna hii hapa chini: Michango ya Baby Shower: Kwa kawaida ukialikwa unaenda na Zawadi inayomhusu Mtoto mtarajiwa si ndio? Sasa hii biashara

Religious vs Believe in God

Nilikuambia nipo Michezoni Glasgow-Scotigo, basi bwana si nkakutana na jamaa wakaniuliza kama mimi ni Religious, nkasema hapana ila naamini Mungu.....acha washtuke!!! Udini unatutenga, Udini unasababisha watu wasifanye mambo kwa uhuru, Udini hukosesha watu wake/waume wema n.k. Hivi unajua kuwa Dini zililetwa na Wageni ambao sasa ama hawazifuati au wameamua kubadilisha waliotuaminisha kuwa "yaliandikwa" na nani sijui nani. Halafu Waafrika tunaanza kuwaona namna gani vipi hawa jamaa wanatubadilishia Maneno ya kwenye Vitabu vyetu vitakatifu ili kuendana na "maisha" ya sasa! Ama kweli Dunia imefikia mwisho. Tunajipa Moyo na kushikilia Imani zetu tukiamini kuwa ni za kweli na kuponda hao Wageni (Wamagharibi na Waarabu waliotuletea hizo Dini) kuwa ni Wafuasi wa Shetwani. Baada ya wao kuchoshwa na Imani mbili tangu Miaka 2000 iliyopita wengi wao wakaamua ama kuachana nazo au kuanzisha nyingine ili ku-suit maisha yao ya Nyakati hizi. Sasa wewe unapoteza Muda wako wote kuja

Review Undugu wako...

Familia/koo nyingi huwa kuna mtu ambae karibu wote wanaMshuku....wanamuona hatari....kutokana na mambo yake Kiuchumi kuwa safi na kila anachosema basi ni "sheria" au hupewa "umuhimu" au "umakini" hata kama alichosema ni upuuzi! Yaani watu kwenye Familia\Ukoo husika hawaishi kwenda kwa huyo mtu, watoto wake, Mke/Mume wake wote wanapewa attention tofauti na akina nyie Hohehahe. Mtu huyu na Familia yake hufurahia yote hayo na huwa on the look out kuona nani anakuja speed ili kuwa kama yeye au kumpita Kiuchumi....basi akigundua atafanya kila alijualo kuzuia Ndugu (tumbo moja) au Jamaa(ndugu wa mbali wale wa kuunganisha mjomba, binamu etc) asifanikiwe. Umewahi kumpa Ndugu yako wa hivyo idea ya Biashara au Mradi halafu akakukatisha tamaa kisha yeye anaifanya hiyo Biashara au ule mradi ambao alikuambia kuwa huwezi kufanikiwa ukiufanya, kwamba utapoteza pesa tu??.....hihihiihi sasa amka na review Undugu wenu! Mtu