Skip to main content

Posts

Ijumaa moja Baada ya Mauaji ya MwembeChai!

Maisha haya! Nimekumbuka 1996/97 Mauaji ya Mwembe Chai (siku mbuki vema na sitaki ku-google vilevile)! Siku chache baada ya Mauaji yale bado kulikuwa na Maandamano ya Siri ya "Waislamu wenye Hasira".....Kile kifo cha yule Kijana pale Mwembe chai akianguka LIVE baada ya kupigwa Risasi na Polisi (FFU sijui) akiwa amevaa shati la Bluu Mpauko(light Blue) kamwe haitonitoka Kichwani! Ni kifo cha kwanza nilishuhudia live(on Tv)!! Sasa bila kujua si tukaenda Kariakoo siku ya Ijumaa! Ile tumemaliza manunuzi si tukakutana na Waandamanaji na FFU...wakayaachia Mabomu ya "Machozi"....oh boy! Nilihisi Vita kuu ya Mwisho wa Dunia ambayo sina Uzoefu nayo ndio imefika!!! Kimbia, huku na kule mara Tukakutana na jamaa (sijui Katibu au Mlinzi, ila alikuwa Mhindi) Wa SSC pale Msimbazi, akatufungulia Mlango kwenye Jengo la Simba....akawa anaita akina Mama na Watoto waende kupata Huduma ya kwanza....hihihihi kunawishwa Maji Usoni(wasn't a laughing matter then)! Anyway! Baada ya hapo k

Kujikanganya nako!

Kuna siku nilisikilizishwa Nyimbo za Bi Rozi Mhando akizungumzia "Kunyang'anywa" Mali zao na Wageni..."Wao kuwa Wageni Nchini mwao". Aliendelea na kuimba kuhusu kuchukua na Kunyang'anya vilivyo vyao kwa Jina la Yesu!.....Nkajiuliza Kunyang'anya(kutumia nguvu) si ni Dhambi?!! Halafu nikakumbuka Ubunge ni Career Path kwa watu Mashuhuri ila issue nzima inayonifanya niandike hapa ni ile ya kuji-contradict!! Isitoshe kuwa Mlokole kwa Miaka zaidi ya 20 lazma utarudi nyuma (utachoka) kumsubiri Yetu (hihihihi my ribs... Wapendwa na Watumishi habari gani?) na hivyo kuhama Kanisa, Kuanzisha Kanisa Lako au kujiingiza kwenye mambo mengine ambayo ni tofauti na Misimamo yako. Si walokole tu wanaoji-contradict kwa kukataa "Mikorosho" lakini wakati huohuo Kumuita Yesu ni Mume wa Wajane (Wajane sio Wanawake tu kama ulikuwa hujui, kuna Wajane wanaume) kwa mfano tu!! Kujikanganya ni kitu cha kawaida ailimradi

Kizazi cha Santuri, Kaseti CD Vs MP3...

Nimekatiza mahali mtaa wa ki-Posh nikakutana na "Bei Nanini CafE" haraka haraka akilini ikaja "Price and what's not"....not exactly what they meant ni mimi tu na Utamu wa Kiswahili.....liwache hili! Unakumbuka enzi zako ulipokuwa unakuwa miaka ya 92+ hapo ndio Tv zinaanza kuchanganya(sio Vituo) bali watu kumiliki Tv(wageni wa Jioni wakapungua nyumbani kwetu). Kila ulichokuwa ukifanya Mzazi wako anakukatalia akisema "enzi zetu tulikuwa hivi na vile....sio nyie watoto wa siku hizi"! Halafu unatamani kumuambia "sasa Mama enzi zako si zimeisha, hizi zetu" lakini huwezi, unaishia kununa. Nakumbuka Baba(Marehemu) alikuwa anasema "hivi huko Madukani hakuna nguo za wakubwa, zote ni za watoto tu?" Akimaanisha zinabana au fupi!....tukamwambia "Baba hii ndio mitindo ya kileo".....alisema "vaeni mtakavyo lakini mkija Ofinisi kwangu sitaki kuona chupi ndefu" (Suruali za Kubana).