Skip to main content

Posts

Lugha ya Mama kwa Mtoto...

Huku (UK) watu ambao tunaongea lugha zaidi ya Moja huwa tunashauriwa kuachana na "local" Lugha na kuwafunza Watoto wetu Lugha ya "mama".....in my case Kiswahili. Kama kawaida ya Mzungu(anajua kila kitu)....wanadai kuwa Mtoto husika atajifunza "local" Lugha (Kiingereza) akianza Shule na hii itamsaidia Mtoto huyo ku-master "Lugha ya Mama vema". Kwenye hili kuna Mawili muhimu(Kichwani kwangu): Mosi; Wanataka mtoto wako awe nyuma Darasani, kwamba akianza shule huku hajui "local" Lugha wanaoijua (wenyewe) wataendelea mbele wakati Mwanao anapoteza muda kujifunza. Pili; Aki-master lugha ya "mama" watamtumia vizuri (hawatoajiri Mgeni wa Lugha yenu) ili kufanya kazi ya Kutafasiri na pia atakuwa kajifunza Bure(hawakulipi kumfunza M-british Lugha yako). Kwanini nawaza/fikiri hivi? Well....Muingereza hana Lugha nyingine zaidi ya Kiingereza, iweje akuhamasishe wewe umfunze mwanao Kilugha chenu badala y

Nanyanyapaa au na-practice

Freedom of expressing my view? Sijui... Alikuwa Mwanaume, akaathirika Kisaikolojia kwa kuishi kwenye Mwili wa "mwanaume" wakati yeye anajijua na kuwa ni Mwanamke. Akaoa na kuzaa ili kuficha "tatizo" lake....akashindwa kuvumilia akawa anaibia Mavazi ya Mkewe na kujiremba mkewe akiwa hayupo nyumbani. Anapenda urembo na kuvaa kama mwanamke, baada ya Miaka kadhaa akaomba "Shirika la Afya" ku-fund Upasuaji ili abadilishe Maumbile na Jinsia na kuwa complete au legally "Mwanamke" . Ombili lake likapita kwa "ground" ya Kuathirika Kisaikolojia na asipofanyiwa Upasuaji(kubadilishwa Jinsia) anaweza kuji-harm.....so akanza Tiba ya Homono, baada ya Muda akabadilisha Jinsia na Documents zote zikabadilishwa kutoka Mwanaume kuwa Mwanamke. Sasa amepata Mpenzi mpya na anampango wa kufunga nae ndoa, Mpenzi huyo ni Mwanamke. Anadai kuwa anavutiwa sana na wanawake hihihihihiihi which make him a real Man(in

Bank Kuu Tz na Gmail account...REALLY?!!

Huenda wana account yao Official ambayo inawawepa mahali pazuri KIUSALAMA online. Nimepokea Email kutoka Bank Kuu ya Tanzania, ikinipa tahadhari kuwa nisipobadilisha "Details" zangu via Link waliyoiweka basi sitoweza ku-Bank Online na Bank yeyote Tanzania! Nikaenda kwa "sender" nikaona mtumaji ni "blablabla BankOfTanzani@gmail.com ".....nkacheeeka halafu nikapachika tusi! Kwanza mimi siBank na Bank yeyote Tz online, Halafu huwezi tu kuwaambia watu wabadilishe "details" zao via link, kwa sababu za Kiusalama kila mtu angepata taarifa hiyo kwenye account yake ya Online ambapo anaingia kwa kuweka "details" ambazo ni zaidi ya jina lake na Namba ya Card, yaani za "siri" na ni yeye tu ndio huwa nazo na hubadilika kila unapo BankOnline. ....aiiii naona nazungumzia System ya huku na sio ya huko Tanzania ambayo siijui. Nachojaribu kusema ni hivi;- Kama ilivyo kwenye Kutongozwa kuna Ma