Skip to main content

Posts

Kutoboa Mtoto Masikio(Kutoga)

Ni umri gani hasa unapaswa kumtoga Binti yako Masikio? Na je yeye kutoga masikio na kuvaa Hereni ni muhimu kwake au kwako wewe Mzazi? Mie nilitogwa nikiwa mchanga (Miezi Sita) na nilichelewa, kutokana na Imani sijui Desturi ya mmoja wa Wazazi wangu ni lazima Binti wa kwanza atogwe na kuvalishwa Dhahabu. Binti yetu alipofikisha Miezi 3 Baba yake akasema tumpeleke akatobolewe(Togwa) Masikio, mie nikapinga na ku-suggest kuwa tumuache na akikua ataamua mwenyewe kutoga au kutokutoga. Nikaongeza, tena atakuwa na kitu cha ku-look forward to, mf: "nikifikisha miaka 15 natoboa Masikio".....kuliko tumalize kila kitu akiwa Mchanga halafu akikua tu tunaletewa Bf au Mjukuu kabisa sababu kila kitu tumekifanya akiwa bado mtoto. Isitoshe (in my head) tunatoboa watoto masikio kwa ajili yetu wenyewe Wazazi, yeye mtoto wala hajali kama anavaa Hereni ama hana "kitobo" cha kuweka Hereni. Baadhi ya Wazazi huku Ulayani wanachukulia kumtoga m

How to be Mum, Wife, HomeMaker and Blogger...

Mimi sijui! Hihihihihihi huyooo unapenda kutafutiwa kisha wee unameza tu (copy and paste)!! Mwanamke mwenye maisha kama yangu (not exactly ila kwa mbaaaali) unawezaje ku-keep up na Blog updates kila siku? Sio blog kama hii ambapo sihitaji kufikiri bali natiririka tu. Zile ambazo unatumia akili kimtindo kwa kuvuta kumbu-kumbu (Uzoefu) na kufikiri.......aiiiii Imenishinda! Basi nimefika nyumbani siku hivi, nawakilisha nilichoambiwa na Walimu wa Babuu.....Baba mtu wacha aanze kung'aka....."Mimi sifuati wanachotaka wao kwenye nyumba zao za Kizungu, nafundisha mwanangu nijuavyo mimi". Nikajiuliza kwa hasira bila kutoa sauti....hihihihi "sasa ni kwanini tunampeleka mtoto shule ikiwa hatutaki kuwa kitu kimoja na Walimu wake?". Nikasema....Asali wa Moyo, shuleni kuna Mihula (mipya imeanza August) na ili watoto waimalize vizuri, kuelewa na kwa wakati ni lazima Wazazi wa-work together na Walimu, vinginevyo mtoto atakuwa

Blogger wapya!

Hellooooo*clear throat*....hi! Kuna kipindi wana-blog (wapya) walikuwa wanasemwa sana, "kila mtu anaanzisha blog" baadhi ya Blogger wakaacha (mie nakaribia kuicha ile ingine maana.....takuambia siku ingine) hivyo naangukia kwenye "newbes" si ndio!!! Kipindi naanza ku-blog 2005(kabla sijawa serious 2007), hao hao walikuwa wakilalama kuwa Watu (Wabongo) wapo nyumba, hawa-blog kama wenzao wa MBELE(hasa Wahabari na Watu mashuhuri). Mara haooooo wote wakawa na Blogs(well baadhi).....kinachoKERA ni kuwa na habari zilezile bila kusema chanzo/Kielelezo. Mambo ya Beauty, Lifestyle, Fashion and News(kila mtu). Aaah! Who cares....maisha ya kila mmoja wetu yapo tofauti na interesting in a way hivyo sio mbaya kuongea mwenyewe via Blog kwa matumaini kuwa mtu mmoja atasoma na kucheka au kujifunza.....asa uta-Copy vipi na Ku-paste mtindo wa Maisha na Uzoefu binafsi ya Mtu? Hihihihihihi lione! Hata hivyo....Mbio zimepungua ila mizung