Skip to main content

Posts

How to(Jinsi ya) kumheshimu Mumeo...

...muendelezo wa Post ya jana, kama hujaiona bofya hapa . Najua ungependa kujua namna ya kumheshimu Mumeo zaidi badala ya kuwa Chini yake si eti? Kama ujuavyo sote tumepetia Mazingira/Malezi/Makuzi tofauti na hivyo hatufanani Kitabia, hivyo basi Kuheshimu Mume nijuavyo mie huenda ni tofauti na ujuavyo wewe.,...sasa labda chukua ambalo ulikuwa hulijui na ongezea kwenye yale uyajuayo? au acha kama yalivyo ila ukiweza share yako na mie "niangalizie". Kumbuka Heshima ni muhimu kwa pande zote mbili lakini leo tunaegemea kwa Mwanaume kwasababu mimi ni eerrrr Mwanamke? also Topic ilikuwa Mwanamke kuwa Chini ya Mwanaume? Sasa kama tumeelewana hapo, twenzetu; Muachie maamuzi Makubwa- Hata kama Kipato chako ni Kikubwa mara Nane kuliko chake, Sio unajiamulia tu kununua Nyumba au kupeleka Watoto Private School kwa mfano..... kwasababu tu unaweza. Mpe Mumeo nafasi na mjadiliane. Unaweza kuweka Mezani aina/sehemu 3 za Shule/Nyumba na kisha muache yeye afanye Uamuzi wa Mwisho kisha

How to(Jinsi ya)...kuwa Chini ya "Mumeo"....

....imekuwa kawaida kwa Wanandoa Wake kwa Wame kutafuta "jinsi ya" kufanya mambo mbali mbali ili kuifanya Ndoa kusimama Imara na kuepusha misuko-suko ya kihisia na hivyo kupelekea Ndoa kuwa Ndoano na pengine kuharibika. Hii kuwa "chini ya Mumeo" hata mie siijui na vyovyote ilivyo kamwe sitokubali kuwa "Chini" ya  Mtu yeyote achilia mbali Mwanaume ila nitakuambia ninachokijua ambacho huenda ni tofauti lakini bado kinamrudishia Mwanaume hali ya kujihisi/sikia kuwa anaheshimika/heshimiwa na Mkwe. Tatizo kubwa linalofanya Wanawake kukumbushwa au lazimishwa na Jamii kuwa ni LAZIMA wawe chini ya Wanaume (asiwe na Sauti) pale wanapoamua kufunga Ndoa ni kutokana na Imani kuwa Mwanamke anaposimama na "kujitetea" na/au kum-challenge Mwanaume basi huesabika kuwa hana Adabu, hana Heshima kwa Mwanaume husika. Ukweli ni kuwa unapokuwa kwenye Ndoa ya "ndio Bwana"  kwamba kila anachokisema Mwanaume wewe unakubali tu....huondoa Changamoto

Kubishana/Fokeana Mbele ya Watoto...

....kuna Ubaya? Baadhi ya watu wanasema SIO vema kwa Watoto wenu kuwaona mkigombana iwe ni Ugomvi Mkubwa(Pesa za Savings acc zimenda wapi?) au ule mdogo(kwa makusudi hujasafisha Bafu). Nyie huwa hamgombani? Kama hamgombani basi mmoja wenu anaishi "kisiri", ulie nae sio yeye...au mmoja wenu anamuogopa mwenzie. Mie ni that Woman ambae nina Sauti kali/ya juu which is a shame kwasababu huwezi kujua kama ninafoka au ninaongea kawaida, sasa ukitaka kuongea kama mimi ni wazi kuwa Utakuwa unanifokea kitu ambacho kitanikera na hapo moto kuwaka...umeona? hihihihihi nataia!! Wazazi wengi hujizuia  kuanzisha "Mabishano" mapema na hivyo, husubiri mpaka Watoto watakapokwenda Kulala ndio wanaanza kubisha/fokeana. Nakumbuka wakati nakua Baba na Mama walikuwa wakifokeana Chumbani kwao(wakiamini tumelala) kumbe some of us (Mie) tulikuwa tunaenda kusimama Mlangoni na kuwasikilia ili tujue kama wanabishana/gombana au wanaongea kawaida tu na kama wanagombana, wanagombania n