Skip to main content

Posts

Muendelezo wa Twiti yangu ya "if he is hot, don't let yourself go"...

Miaka mitatu iliyopita niliandika kuhusu Wanaume wapenda nachuro byuti, kama ilikupta isome hapa  kisha tuendelee. Kwanza habari za leo? mie nipo Likizo, aina ya Likizo ambapo unafanya yote uyafanyayo unapokuwa nyumbani isipokuwa haupo nyumbani. Achana na hili. Kuwa shabiki wa "natural beauty" wakati unavaa Nguo, unaoga maji Safi ya Bomba(yana Kemikali), unavuta hewa kila siku(imejaa toxic), unakula vyakula vinavyotunzwa kwa kutumia Kemikali ili kuepusha magonjwa/wadudu, Ukiugua unatumia Tiba ya Kisasa, Unatumia Simu kuwasiliana  n.k. sio rahisi. Hakuna tatizo la mtu kupenda Urembo wa Asili na hakuna tatizo kwa yeyote anaependa Urembo wa kununua/jiongezea ailimradi tu hambadilishi na kukufanya uonekane mtu mwingine. Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wanaume kusakama Wanawake wanaopenda kujiremba(usually wasio kuwa na pesa, maana makeups sio chee). Kutokana na maisha yalivyo  hivi sasa (Wanawake tunafanya yaliyokuwa yakifanywa na Wanaume pekee) na mabadiliko ya Hali

Kuwa "affectionate" kwa Mwenza wako kunaweza haribu Ndoa/Uhusiano wenu...

Baadhi ya watu hasa Vijana wanapenda sana kuonyesha "hisia" zao kwa vitendo, katika umri mdogo ambao ndio kwanza unajifunza Ujinsia wako, "Affection" goes a long way. Katika hali halisi huitaji zaidi ya kuhisi unapendwa na  kupata uzoefu wa mwili wako unavyoibua Msisimko wa raha ambao hujawahi kuuhisi tangu Ubalehe/Vunje Ungo. Wengi huamini wapenzi wanaofanya hivyo basi huwa na uhusiano/ndoa yenye Afya. Ukweli ni kuwa sio mara zote, sio tu kwamba kuna wakati mnajikuta hamna muda kutokana na mtindo wa maisha ya sasa bali inapoteza uzito/umuhimu(ni vema kuirudisha time to time). Utajiuliza kwanini kuonyesha "hisia" zako kwa vitendo kuharibu uhusiano/ndoa wakati ukifanya hivyo unajisikia vizuri/raha na kuwa karibu zaidi na mwenza wako? Jibu ni rahisi tu, Kwenye Ndoa kuonyesha Hisia zako ni rahisi kuliko kukabiliana na "issues" kubwa au hata  kuchangia maoni yako au kumshauri mwenza wako labda kikazi, kifamilia(kule alikozaliwa), maendeleo n

Dini inaweza kuyumbisha Ndoa/Uhusiano wako....

Heri ya J'Nne, Kama nilivyokuahidi Wiki (mbili na Siku Moja) iliyopita (bonyeza hapa kama ulipitwa) kuwa nitakuja nikukumbushe tu ni kwa namna gani Imani yako ya Dini inaweza kuyumbisha Ndoa au Uhusiano wako. Kwa kawaida wengi hudhani kuwa mtu anapokuwa Mumini Mzuri wa Dini au "anamuogopa" Mungu ndio atakuwa muaminifu, atampenda kwa dhati, atakuwa  mkweli, hatomuumiza na mengineyo mazuri mazuri. Ukweli ni kuwa Mtu wenye Dini mara nyingi huwa mwepesi kutenda "dhambi" au yale ambayo hayaruhusiwi na Dini zao akijua kuwa atasamehewa, sio tu na Mungu bali wewe Mwenza wake unapaswa kumsamehe. "Ikiwa Mungu aliemuumba anatuambia tusamehe iweje wewe ushindwe kunisamehe". Mazoea hayo ya kutegemea kusamehewa kila unapofanya makosa ya makusudi hupelekea upande mmoja kuhisi upweke na kuondoa Amani na Furaha kwenye Uhusiano /Ndoa. Hii inaweza kupelekea kujitenga na pengine kutafuta furaha Nje ya Muungano wenu. Hilo moja. Pili, Imani yako ya Dini inak