Wednesday, 25 August 2021

Nguzo 5 za Mahusiano bora(Masikilizano/Maelewano).

Masikilizano/elewano huja wakati/baada ya mawasiliano japo ni Nguzo inayoweza kusimama peke yake kutegemea na tukio....mf:- wakati wa manunuzi makubwa(gari, nyumba), familia yenu iwe na watu wangapi?, Shule/Malezi ya watoto na pengine “career”.Unapowakilisha jambo/kero kwa mwenza wako ni vema kuwa katika hali ya utulivu(sio mara zote hufanya kazi hasa kama mwenzio sio msikilizaji mzuri). Utulivu wako husaidia kutoongea kwa sauti ya kushambulia na hivyo kuepeuka yeye kujitetea(bila shambulio hakuna pa kurudisha shambulio).Unapoibua suala ili lizungumzwe/jadiliwe nia ni kufikisha Ujumbe/kero na kupata muafaka(maelewano) na sio kung'aka na kuanza kugombana....hii hupoteza muda(kusumbua watoto kihisia/akili) na tatizo kuzimishwa badala ya kumalizwa.Kuzima/acha tatizo bila muafaka/maelwano kwa muda mrefu hupelekea mwanzilishi wa “mazungumzo" kuhisi kuwa hasikilizwi na hisia zake hazithaminiwi na mwenza wake.Hisia hizo hupelekea hasira(jitahidi kujizuia ili usifanye jambo mbaya) na pengine kupunguza Heshima kwa mwenza wake.


Kutoelewana/sikilizana pia hupelekea “issues" kurundikana kitu ambacho sio afya kwenye Uhusiano wenu.Suala muhimu hapo ni Msikilizaji ambe hakusikiliza na badala yake kuanza kujitetea kwa kung'aka(na kutimia maneno  makali ya kuudhi) kuomba radhi.Siku nyingine, jaribu kuomba mzungumze na kumwambia mwenza wako kuwa “naomba tuongee kuhusu blablabla, usikilize kwanza mpaka mwisho bila kufoka, kujibu wala kunikatisha.Heshima ikikosekana kwa pande zote mbili, Uhusiano unaweza kuyumba na pengine kufa. Heshima ni Moja ya Nguzo muhimu. Njoo tena ukipata muda, tuiangalie Heshima kwa “engo” tofauti na ile ya 2015.....Muda wako unathani kubwa kwangu, ahsante.
Bai.

Sunday, 15 August 2021

Nguzo 5 za Mahusoano/Ndoa Bora...

Nguzo 5 za Mahusiano bora ya Kimapenzi ilikuwa topic maarufu sana 2007. Unakumbuka?


Nilizielezea kwa kirefu kama utambulisho, wakati ule wengi walikuwa hawafahamu na baadhi hawakuwa wameziishi.


Sasa tangu umeziishi nineona sio mbaya kama nikizirudia tena kwa pembe tofauti kidogi na ile ya 2007.


Kabla sijaenda huko hebu nikukumbushe Nguzo hizo ambazo ni...

1) Mawasiliano.
2) Maelewano/sikilizano
3) Ushirikiano
4) Heshima
5) Kujali


Ni rahisi kudhani kuwa wewe na Mwenza wako mnafanya yote hayo na kuamini kuwa Uhusiano wenu upo Imara.


Utajuaje kuwa Mawasiliano ni mabovu?

Mara ya mwisho kukaa chini na kuzungumza masuala yenu binafsi na yale ya kimaendeleo?


Je, mwenzako anapokuja na hoja, huwa unasikiliza, jadili inapobidi na kufikia maelewano? 


Ikiwa Mara zote mnaishia kubishana badala ya kujadili sababu mmoja wenu kapandisha sauti(foka) basi ujue uhusiano wenu hauna mawasiliano.

Ni muhimu kutafuta namna ya kurekebisha na kuboresha kona hiyo.

Njoo tena tuseme kuhusu Masikilizano kwa pembe tofauti na ile ya miaka 14 iliyopita. 

Nathamini Muda wako, ahsante. 

Bai.

Tuesday, 10 August 2021

Uviko nusura uue Viungo vya Uzazi...

...umesikia mengi kuhusu mabaya ya Uviko kuanzia upumuaji, vifo, ukosefu wa pesa/kazi, mpaka ongezeko la kuvunjika kwa Ndoa(Talaka).

Inaonekana wanandoa wengi walikuwa hawajuani, sasa baada ya kulazimika kukaa pamoja masaa 24 kwa zaidi ya miezi 3 wakagundua Wenza wao sio Wenza wao tena.


Mf;  kwenye baadhi ya Ndoa wamegundua hakuna mawasliano kati yao. Au Mume kapoteza "value" sababu  sehemu ya majukumu yake (kulinda, kutunza/lisha) yamechukuliwa na Serikali.


Hata kama Mke alikuwa "working mama" kabla, Majukumu yake kwa kiasi kikubwa yatabaki palepale. Tofauti na mwenza wake.


Hakuna kitu kinaondoa mvuto kama Mwanaume kutokuwa na Shughuli ya kumuingizia Pesa...hii hupelekea kupoteza takwa lamwili na hivyo ukosefu wa Tendo na hivyo watu wakaanza kushi kama "housemates" na sio wanandoa.


Kwabaadhi yetu hali haikuwa mbaya hivyo, sema tatizo lilikuwa Vitakasa mikono. Kwasababu ya uoga(na uvivu wa kwenda kunawa mikono kwa maji na sabunu mara kwa mara) matokeo yake unapeleka mikono "kunako" kunogesha hisia...kesho yake unaanza kuwashwa sirini.


Unajiuliza Jamaa kaniletea gonjwa la zinaa? Ila kalipataje na tuko pamoja 24/7 mwezi wa 9 huu. Kumbe ni "irritation" ya Vitakasa Mikono.

Nathamini muda wako, ahsante.
Bai.