Skip to main content

Posts

Showing posts from February 13, 2022

Amina wa Ali Kiba adai Talaka Mahakamani na Kiba(2)....

Soma Mosi na Pili hapa .... Tatu, Mtoto anamuhitaji Mama yake full time kwa Miaka 5 ya mwanzo ya Maisha yake baada ya hapo PT sio mbaya. Malezi ni Kazi  kama kazi nyingine na inachosha Akili na Mwili, tofauti ni kwamba hakuna Likizo na huwezi kuacha/badilisha na pia kwa  Tz Mke (Mama wa Mtoto) huwa halipwi na hiyo inafanya kuwa "Kazi" hiyo kuonekana kuwa ni rahisi. Mkeo anapoamua au mnapokubaliana kuwa yeye abaki Nyumbani kulea watoto ni jambo zuri na la kuheshimika kwa Ulimwengu wa sasa. Mkeo akigoma kufanya Kazi ya Kulea na kuamua kwenda kufanya kazi/biashara nje ya nyumbani ni wazi kuwa mtahitaji "Mlezi" wa watoto wenu wa hapo nyumbani na yule wa "shule", na atalipwa kwa "rate" nzuri tu kulingana na Kipato/aina ya Maisha mnayoendesha. Wengi kwenye Mitandao wamelichukulia suala la Amina na Kiba kwa kuangalia Kona ya maisha waliyonayo wao kwa sasa, na sio Maisha ya Star Mkubwa mwenye Thamani ya Dollar  Millioni 5(11,570,000,000). Pi

Talaka ya Amina kwa Ali Kiba...

Mimi na wewe hatujui kwa Undani ni kitu gani hasa kilichopelekea wawili hao kufunga Ndoa 2018. Lakini kutokana na Maelezo ya Amina kwenye Hati ya Madai tunajua kuwa Kiba alikuwa Mtesi/Mnyanyasaji kwa Mkewe (Kiakili, Kimwili, na Kisaikolojia)baada ya Miezi 6 ya Ndoa. Kwa maelezo hayo inaonyesha kuwa Amina hakuwa "kipenzi" cha Familia ya Mumewe na hivyo kuhisi kuwa mahali walipo watu hao sio Salama kwake na kwa Watoto na hivyo kurudi kwao Mombasa*. Pia Amina ameongeza kuwa Mumewe(Kiba)ni Muasherati na hakuiheshimu yeye(Amina) wala Ndoa yao(alimdhalili adharani). Amina amedai kiasi cha Laki mbili kwa mwezi(Ksh) kwa ajili ya Matunzo yake na watoto. Madai ambayo yamesababisha Watanzania wa Twita kuhoji... Tu(na)jigunza nini kwenye tukio hilo. Moja, Kwa Msanii mkubwa kama Ali Kiba ambae ana Thamani ya Dollar Millioni 5(568,500,000Ksh) Laki mbili kwa mwezi kwa mahitaji ya Mtoto sio pesa nyingi, pengine haitoshi tukiongeza Ulinzi, Usafiri na Bima ya Afya.  Unalipa Matunzo

Hebu tuone Past life yako: Kuachwa/Telekezwa(2)...

Jambo, ni furaha iliyoje kukutana nawe na ahsante kws kuwa nami leo. Naendelea kukumbusha Maisha uliyopitia ulipokua angali mtoto ili kuona jinsi gani yana athiri Maisha yako hasa kwenye Mahusiano na watu wengine. Kuachwa ni jambo ambalo limezoeleka sana kwenye Jamii(hata za Ulaya ya hapa), kwamba utaachwa, utalia weeee kisha utanyamaza halafu Mzazi akirudi hautokumbuka tena(asiporudi tena baada ya miezi 2? Miaka 3?). Imani hiyo hufanya Wazazi wengi kufanya maamuzi yanayo umiza mtoto(hukumbuka ila hawajui ku-express hisia zao) bila kujua(kwa sababu hata wao walifanyiwa hivyo na they turned out just fine hivyo its okay). Kuachwa/Telekezwa na Mzazi kunafananaje? Mama ambae anamnyima mtoto Nyoyo kwasababu nyingine hana tofauti na Baba ambae hajihusishi (hayupo)kwenye maisha ya mtoto.  Mzazi aliefariki wakati kabla  hujazaliwa/angali ukiwa Mdogo....athari ni zilezile. Na je ni Matendo gani yanaashiria kuwa uliachwa/telekezwa na Mama/Baba na umeathiri? 1-Unapenda "attentuon" na ku