Skip to main content

Posts

Showing posts from April 12, 2015

Faida ya kumchukia mtu usiemjua....

Ni nini hasa? Unajua kuna watu maisha yao ni ya huzuni sana bila wao kujijua. Anakaa kabisa na kutulia kisha anaanza kurusha maneno makali. Unawezaje kum-attack mtu kwa matusi wakati humjui? Hupendi anachokiandika au kukisema fair enough....sasa kitu gani kinakupeleka kwenye Ukurasa wake wa FB au Twitter au Blog na Sites? Binafsi kama sipendezwi na Blog fulani basi sitoitembelea tena.....muda wa kuendelea kufuatilia anachokiandika ambacho mimi sikipendi sina. Heri nitumie muda huo kupeleka Wanangu Park wakacheze au nikoshe nywele zangu au kutengeneza Kucha au kwenda kufanya manunuzi at the end nifurahi moyoni......there are so much more in life than being a Troll. Unakosa usingizi ukifikiria nini cha kwenda kumuambia mtu in an attack way kwenye Site au Page yake.....unapata faida gani? Mimi Dinah kuacha kublog Dinahicious is nothing to do with January Makamba au mabadiliko ya Sheria Tz ni uamuzi binafsi. Ngoja nikusaidie kuelewa: Google walipokuja na mabadiliko ya Sheria Mwezi w

Namba ya Simu imekuwa too personal....

Heyaaa! Unawajua wale watu wanagawa namba yako ya Simu kwa watu wengine bila idhini yako. Tangu enzi mie nachukulia namba yangu ya simu ambayo haihusiani na "Kazi" ni personal na hakuna mtu anapaswa kuwa nayo isipokuwa wale ambao nadhani ni muhimu maishani mwangu kama sio leo basi huko baadae. Sasa kutokana na Maendeleo ya Kitekinolojia Simu si ndio zimezidi kuwa PERSONAL kuliko namba? Halafu unashangaa kwanini watu wanaweka Passwords au PIN ku access simu zao. Nilipopata simu yangu Mpya (kumbuka nimekuwa nyuma na  Teknolojia ya  Simu kwa Miaka 3.5)....so niliponunua ze latest simu si ndio ikanishtua. Ile mambo ya urahisi wa kupokea na kutuma Emails mdio ikanitisha kabsaaa. Nime add Email address nikaletewa the whole thing.....kumbuka sijagusa emails via desktop kwa miaka sasa nilipoona mafolda yaliyokontaini barua za wapita njia na some picha zao dated back in 1999 to 2005 si nikapata Mini heart attack! Nikabonyeza futa daima milele. Zaidi ya hizo kuna zile unasubiri m

Jaribio.....jaribio la Picha!

Tatizo...kila nikiambatanisha Picha Post inagoma ku-publish. Nimapunguza ukubwa....nimebadilisha settings lakini Ola!  Nimeambatanisha picha kwenye post ya jana lakini haionekani....kwenye hii pia nimeweka picha. Heeeelp tafadhali. Ahsante.

The other woman kwa Kiswahili ni Kimada?

Jana nilikuwa masoma Magazine moja hivi nikakutana na stori ya mdada Mashuhuri kiasi cha kutosha Uingereza. Alikuwa akizungumzia suala la kuwa Kimada ukitumaini au kuomba kama sio kusubiri Mwanaume unaemuiba amuache mkewe na watoto wake ili mwanaume huyo awe na wewe full time. Akaongeza....Mume wa mtu alipomtokea kabla hajajua kuwa ni mume wa mtu alimkubali then Jamaa akamwambia ameachana na Mkewe na Talaka itachukua muda  kiasi hivyo sio mbaya kama wakilianzisha. Mkimama akagoma na kumwambia watatoka soon baada ya Talaka kukamilishwa kwasababu hataki kuwa sababu ya kuharibu Maisha ya Mkewe na Watoto wake. Akagusia kwa kusema....wanaume  Wazinzi huanza kukuvuta kingono via mitandao ya kijamii na kuomba uwaambie utawafanyia nini ikiwa utapata nafasi ya kuwa nao. Kisha huenda na kuponda maisha yao ya kingono na Wake zao kwako.....halafu wakiona upo interested wanaongeza "i wish my wife angekuwa open minded kama wewe"(wakati uliyomwambia ni masuala ya kawaida tu ambayo kila

Sio wote Ughaibuni tulifika kwa Ndege....

Mabaharia.....I see ya! Mambo vipi lakini(i sound like a male)? Ahsante kwa kuichagua Blog hii. Ujue huku nje ya Tanzania kila mtu anauchungu wa maisha kivyake kutokana na sababu zilizomleta....sio mnatujaji kwa kutujumuisha bana. Kuna wale walikuja kuongeza Elimu ili wakirudi waitumie ilimu yao ya kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi yao Tukufu Tanzania. Halafu wapo waliochukia maisha yao yalivyokuwa Bongo na kwa hasira kutaka kwenda kujaribu au kuanza upya huko kwingine.....hawa kurudi sio chee(as in rahisi). Wengine walipelekwa na Wazazi wao baada ya kuanza tabia mbaya na zenye kutia aibu Wadhifu....sasa ili Wazazi waendelee ku-keep Status.....er ya Uchungaji wa Kanisa, Ukuu wa Jeshi au Uwaziri n.k so unapelekwa Nje ukafanye Umalaya wako kwa nafasi. Pia kuna akina sie tulioletwa huku kama Mtaji au Urithi.....kwamba Wazazi wanatumia Akiba ya familia ili ukasome na ukimaliza na kuanza kazi ama ulipe Deni na Riba au uwasaidie Nduguzo ambao technically umetumia Mgao wao wa Urithi

Come to terms with your Uchibonge....

Hello! Naweka viraka mbinguni ujue(mekuwa busy namna hiyo). Mwisho wa wiki nilipata wasaa wa kupekua pekuwa YouTube na huko nikakutana na "how to gain weight".....nikabofya na kuanza kusikiliza hadithi moja baada ya nyingine kuhusu Wanawake wanaotaka sana kunenepa. Unajua unapomsikiliza mtu au kusoma hadithi yake na kuhisi kuwa anakysemea au kukuwakilisha wewe? Yaani anakugusa kumtima. Nikakumbuka jinsi nilivyokuwa Chikonda (skinny)enzi zile nakua(nimeacha kukua nilipofikisha miaka 25 nadhani). Story Time: Nilikuwa mwembamba kiasi kwamba baadhi ya watu walidhani nina Ugonjwa. Mmoja wa Binamu zangu alikuwa akiniambia "mtu mwenyewe maiti wewe.....umebaki mifupa tu". Nilipofika late teen baadhi ya watu Familiani wakawa wanasema ninatoa mimba sana wakati sikuwa namjua mwanaume sasa sijui Mimba ziliingia kwa Roho mtakatifu! Wengine walisema naiga Uingilishi figa na hivyo kutumia madawa ya kujikondesha. Nilichoka kusakamwa kwa uchikonda wangu ambao sikuuom