Skip to main content

Posts

Showing posts from October 19, 2014

Vita dhidi ya Ebola imeSiasa-iwa!

Kila mtu anakuja na lake, mara Wazungu wametengeneza Ebola ili "kumaliza" Kizazi cha Weusi(Waafrika)...huyu ni Mwafrika/Mweusi aweza kuwa Manasiasa au Mtaalam(daktari) n.k. Mzungu wa kawaida (mtaani) anahoji Kwanini mnahaha na Ebola iliyoua watu Chini ya Elfu Kumi wakati Malaria inaua Mamilioni ya Waafrika kwa siku? Vipi kuhusu HIV na Umasikini ambavyo vinaondoa mamilioni ya Watu....TB je? Karibu Miezi Nane tangu mlipuko "mpya" wa Ebola kuibuka(according to my kumbukumbu) Wamagharibi walielekeza nguvu zao Ukraine na Iraqi ambako kuna faida zaidi ya kuokoa Maisha ya Muafrika, Afrika.....mara boom wanapigana zaidi kuliko wenye Tatizo (waafrika)?!! Mwenyewe jana nikajiuliza, kwanini US, EU na Cuba (is Cuba....never mind) wanapeleka "jeshi" la Wataalam kupigana na Ebola which ni more expensive kuliko kupeleke Vifaa na Wataalam wachache wa kutoa mafunzo kwa Locals (Waafrika). Nikapata jibu kuwa, labda Wazungu wanajua w

Kwanini Mtoto awa wa Baba?!!

Nimekaa hapa nikafikiria(sio kweli)....limenijia tu kichwani. Kwanini tunaaminishwa kuwa Mtoto akizaliwa ni wababa, Jina lake la ukoo lazima liwe la Upande wa Baba. Ukimpa mtoto jina lingine la mwisho....baba anakuwa Mkali au anahoji kama kuna "mwenzie"! Kutokana na Mfumo Dume, nahisi(in my head) kuwa wali/na lazimisha hivyo kwasababu walijua/wanajua kuwa Baba ana sehemu ndogo sana kwenye Uumbwaji wa Mtoto. Baada ya zile Dakika Tatu (if you are lucky that is) kazi yake (baba) imeisha, isitoshe Mbegu hazina Damu so mtoto kuwa na Damu ya Baba yake ni kama 0.5% hihihihihi (lazma mnipige mkinikamata wababa). Hebu angalia suala hili kwa undani kwenye jamii bila kuhusisha Sayansi wala Dini! Kwanini hasa Babaz au ndugu Upande wa Mwanaume ndio huwa na viherehere vya kuendeleza Undugu kama sio kujishtukia kuwa hawana undugu (wanalazimisha). Stori time: Kuna siku nipo shereheni, mkaka mmoja akaanza kutambulisha ndugu wa Mama mbali-mbali l