Skip to main content

Posts

Showing posts from February 14, 2016

Kujua kila Kitu vs Kujua kila situation ya Watu....

....nirahisi kupatwa/kabiliana  na mengi kwenye Maisha yako na hivyo kujifunza zaidi, kuliko kujua kila situation ya mtu, achilia mbali watu ambao sio wewe. Niliwahi ku-blog kuhusu tabia ya watu "kujifanya" wanamjua kila mtu au zaidi "celeb" na life situations zao. Hakika hilo linawezekana, lakini ni vema kuweka wazi kuwa unayajua hayo yote kwasababu ya kusoma Gossip Sites/Blogs/TvChanells/Vijiwe/Joints n.k. na sio kwamba unawajua hao watu individually. Kutokana na Maendeleo ya Kiteknolojia,  mawasiliano yamerahisishwa na hivyo baadhi yetu huwa tunapata Majibu/Ushauri wa Maswali/Matatizo yanayotukabili papo kwa hapo. Urahisi huu unafanya wengine kupitiliza kwenye kuchangia "uzoefu" wao kwenye "situations" nyingi kwenye Sosho midia husika na hivyo kukera baadhi. Mie binafsi nina majibu mengi zaidi kuliko your "normal" Dada, kwasababu pengine n iliyopitia mimi kwenye maisha yangu na kujifunza au kupambana na kutatu ni tofau

Mtoto "anaechagua" Vyakula....

....ndio mnaita "Fussy eater" eti? Baadhi ya Watoto huanza mapema(au wazazi wao wanaamua kuwa watoto wao ni fussy kama sifa) katika hali halisi ni Uchovu unaopelekea kutokuwa na utararibu wa "kula" na attention ya kutosha kwenye kula kwa mtoto husika! Kamwe sitokufunza namna ya kule mwanao, isipokuwa nitachangia uzoefu wangu ili kwa namna moja ujione kuwa haupo peke yako na hivyo kupata nafuu na pengine kuchukua "tips" na kujaribu ili mwanao apate virutubisho vyote Asilia ambavyo ni Muhimu kwa Ukuaji wake. Mwanangu wa Kwanza(Babuu) alianza kula Vizuri sana akiwa na Miezi Sita, alipofikisha Mwaka na Miezi 3(Miezi 15) akacha kunyonya mwenyewe(bila kuachishwa). Babuu alikuwa anakula kila aina ya Chakula unachompatia. Alipofikisha Miaka 2 hali ikabadilika, akaanza kukataa Nyama na Samaki which was Okay kwasababu alikuwa akila Mayai vema. Alipofika Miaka 2 na Nusu akawa anakula Viazi tu.....tena viwe vimepondwa(mashed). Ukichanganya Mchuzi au Mbog