Skip to main content

Posts

Showing posts from June 12, 2022

Kwaheri Social Media(Twita)...

...hivi YouTube inahesabika kama Sosho Midia?  Kama sio basi Platform pekee naiaga kwa sasa ni Twitter. Sijawahi "kujiunga" na Instagram, Snapchat wala Tiktok. Kwanini? Ukiachilia mbali kuwa Muda unabadilisha watu(wanakua), vilevile vitu na mitazamo hubadilika kulingana na Tabia Uchumi/Nchi/Utamaduni....nadhani Twita imejaa wafanya Biashara kwa kupitia Ajenda binafsi/Harakati, Biashara ndogo ndogo na Biashara Utapeli (ulipie waliojifunza YouTube  bure), Biashara ya Miili(intimate picha/vid) oh bila kusahau Biashara ya "kuomba omba". Baada ya miaka kadhaa, nimegundua kuwa Twita hainifaidishi kwasababu sina Biashara(sikuzi Brand), hivyo sihitaji kuwa active na ku-engage na followers every few hours on daily. Kabla ya hapo nilikuwa Active sana kwenye Masuala ya Kisiasa(Naunga Mkono Upinzani Tz), baada ya Muda nikajitoa, uamuzi uliopelekea  "kurukia" zaidi issues rahisi rahisi ambazo zimejaa chuki/vita ya Wanawake vs Wanaume, hasira, kutokujiamini,