Kipajiiii....heri ya Alhamisi!
Nilipokuwa Msichana 10-17 sikuwa najali mambo ya kujiremba....Mama hakuturuhusu kupaka Rangi ya Kucha Ijumaa kisha tuondoe J'pili jioni. Eti tulikuwa tunaharibu Rangi zake...
Basi tukawa tunapaka Wino mwekundu(Pen nyekundu) au ukitaka Rangi "clear" au kucha zing'ae basi unachukua Marumaru au Vipande vya China (sahani, vikombe n.k vilivyovunjika) unasugua kwenye Sakafu ya Sementi kisha ile vumbi yake unaisugua kuchani.
Nilipofikia Miaka 18 nikaanza kupaka Wanja na Lip gloss. Nimeanza kujipangusa Poda usoni, kutinda Nyusi na kupaka Mascara nilipokuwa na miaka 28....anyways!
Baada ya kuwa addicted na Beauty Vlogger nikaamua kujitutumua kwenye kujiremba bana....basi siku ambayo najua sitoki nje mwenyewe napanga nitakavyo vyaa the next day na Vipodozi gani vya kujipaka....(Ninavyo kibao kwani kila Birthday napewa zawadi ya Vipodozi....watu wachokozi)!
Naamka mapema, nafanya shughuli zangu za ndan...