Skip to main content

Posts

Showing posts from March 27, 2022

Dayaspora na Uraia Pacha...

Natumai unamalizia vema Mwezi huu wa 3(na Dayaspora). Suala la Uraia pacha ni zuri sana na lina faida nyingi kwa pande zote Mbili za Watanzania(Ndani na Nje), na Taifa lenyewe kwa ujumla(hasa kwenye Michezo Kimataifa, Uchumi, Afya na Elimu). Uwekezaji? Sio sana kwasababu kama Mtanzania utataka "kupendelewa" au "kupunguziwa" Masharti kutokana na Uraia wa Taifa hilo la Uzawa wako na hivyo Serikali kupoteza Mapato(Visa ya Uwekezaji na gharama nyingine) kutoka kwa Wawekezaji wa Kigeni.  Dayaspora wengi wanadhani kuwa Serikali inakwepa suala la Uraia Pacha kwa sababu ya Wivu, Chuki au Uoga wa "kupitwa" Kimapato, Ujuzi na Uzoefu. Kwaharaka haraka(uvivu wa kufikiri) inawezekana kweli ni Roho ya "kwanini wao", lakini ukiamua kutulia na kwenda ndani, utagundua kuwa  Taifa(Serikali) itapa Hasara zaidi kuliko mnavyorembesha Faida za Uraia Pacha. Hasara za Uraia Pacha zipo nyingi ila mie ninazo Nne tu. Tangu kupata Uraia wa Tanzania ni rahisi(kwa sababu ya M