Habari...
Mkorogo ni kutumia bidhaa "illegal" au "home made skin lightening" na "kujiton" ni kutumia bidhaa zilizothibitishwa na Jamaa wa Ubora wa Viwango eti?.....wote nia yao Moja.
Waafrika kwa Waafrika kwa ubaguzi wa rangi zetu hatujambo....tofauti ya Ubaguzi wetu sisi Watanzania ni kuwa hatutengani au kuuana kwa sababu baadhi yetu ni weusi sana au weupe sana.
Well, isipokuwa kama wewe ni Mweusi tii alafu huna nywele laini na unaishi Somalia au Sudani Kaskazini.....oh au Chotara ndani ya South Africa.
Ila Machotara ndio huwa wabaguzi zaidi kwa Weusi kuliko sisi wenyewe kwa wenyewe....Usiombe ukutane na Chotara wa Kizungu aliekubaliwa kwenye jamii ya Kizungu ayeee!!
Anyway, nukta hapa ni kuwa tofauti ya weusi wetu wa ngozi ndio hutufanya tuwatanie wenzetu na kuwaita majina....Mf: Cheusi dawa, Mpingo,Cha usiku n.k
Huu utani huwafanya baadhi(hasa wanawake) wajisikie wanyonge, hawavutii....inafikia mahali wa...