Skip to main content

Posts

Showing posts from June 25, 2023

Jinsi ya kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu!

Kumbuka sababu kuu ya ninyi kuwa pamoja ni mapenzi na sababu ya kufunga Ndoa ni kwavile mnapendana na mnataka kuishi pamoja kwa furaha. Ulipenda na ukataka kupendwa na kufurahia Muungano wenu. Sasa kama hiyo ndio sababu kuu, kuna umuhimu gani wa kuendelea kuishi Maisha ya ndoa wakati hakuna furaha? Utasema Mapenzi, kwasababu mapenzi hayaishi obviously, jinsi mnavyozidi kuishi pamoja ndivyo ambavyo unapata sababu nyingine nyingi kwanini unapenda Mume/Mkeo.   Kuna wakati unaweza usipendezwe na mumeo/mkeo kutokana na matendo yake au kutokana na jinsi alivyokujibu/ongea nawe au kafanya jambo Fulani hukubaliani nalo, hii hali hutoweka mara akiomba radhi au wewe ukiamua kudharau. Hali hiyo haiondoi mapenzi yako kwa mume/mkeo.   Ule msemo wa watu wa social media kuwa “my happiness comes first” au “I choose me” ni kwa wale ambao hawana Imani (hawamuogopi Mungu) ni single au wapo kwenye Ndoa mbaya za unyanyaswaji, vipigo, mateso na masimamngo. Sie wengine ambao wenza wetu wamebadilika sab