Skip to main content

Posts

Showing posts from September 21, 2014

Bank Kuu Tz na Gmail account...REALLY?!!

Huenda wana account yao Official ambayo inawawepa mahali pazuri KIUSALAMA online. Nimepokea Email kutoka Bank Kuu ya Tanzania, ikinipa tahadhari kuwa nisipobadilisha "Details" zangu via Link waliyoiweka basi sitoweza ku-Bank Online na Bank yeyote Tanzania! Nikaenda kwa "sender" nikaona mtumaji ni "blablabla BankOfTanzani@gmail.com ".....nkacheeeka halafu nikapachika tusi! Kwanza mimi siBank na Bank yeyote Tz online, Halafu huwezi tu kuwaambia watu wabadilishe "details" zao via link, kwa sababu za Kiusalama kila mtu angepata taarifa hiyo kwenye account yake ya Online ambapo anaingia kwa kuweka "details" ambazo ni zaidi ya jina lake na Namba ya Card, yaani za "siri" na ni yeye tu ndio huwa nazo na hubadilika kila unapo BankOnline. ....aiiii naona nazungumzia System ya huku na sio ya huko Tanzania ambayo siijui. Nachojaribu kusema ni hivi;- Kama ilivyo kwenye Kutongozwa kuna Ma

Misinformation za Online nazo.

Hellooooo! Urahisi wa kuweka chochote online kwa nia ya ku-share au "kuelimisha" wengine ni mzuri sana! Sote tunajua kuwa kwenye kila kitu kuna Faida na Hasara zake, kama Mwanadamu unatakiwa kupima na kufanya uamuzi kwa kuzingatia faida zaidi (utafaidika?). Sio sote tuna-share yote(kila kitu) online....kwenye Blog ya D'hicious nimeshare mengi tu ila sio yote nijuayo (mengine naweka kwa ajili yangu mimi binafsi) na Binti yangu na Mwanae huko mbeleni Ntakapo kuwa Proper Bibi. Hali kadhalika kwenye Blog nyingine Mf za Urembo, Fashion hufanya hivyo pia....tena hawa huwa hawabani some info, wanakudanganya kabsaaaaaa(wanapindisha ukweli) ili uogope au ukosee na hivyo usitokee as Mrembo kama wao wanavyoonekana au Nywele zako zisikue kama zao. Safari yangu ya Nywele (nilishawahi kukuambia about) imenifanya nijaribu Mengi, kukosea Mengi na Kujifunza Mengi halafu nikarudi kwenye "rutini" yangu ya enzi ambayo kabla ya YouT

Kabla ya Mobile Simu na Net....

Ulikuwa unafanya nini na muda huu unaotumia Simu yako au Mtandao eti?!! Jinsi Teknolojia inavyozidi kukua ndivyo ambavyo maisha yanazidi kuwa busy na kuhisi muda haukutoshi (Masaa 24 yamekuwa machache). Binafsi nilichukua hatua ya kutoka Mtandao mmoja wa Jamii na Kujiunga na ambao ni latest one (Mwisho ilikuwa Twitter karibu Miaka 5 iliyopita) hivyo sikuwa kwenye Mitandao Saba ambayo ingenichukulia Muda wangu mwingi. Kabla ya hapo hakukuwa na Mitandao ya Kijamii, kulikuwa na Forums na Chatrooms pamoja na kuwa nilikuwa na Muda mwingi bado sikujiunga na kila Forum/Chatroom iliyojitokeza. Hapa juzi nimemsikia Business Woman akisema ameamua kufuta Email address yake na baadhi ya namba za Simu za Ndugu, Jamaa na Marafiki wasio na Mpango (wasiomsaidia kwenye Biz yake) ili aweze ku-focus zaidi kwenye Uzalishaji na Uendelevu wa Kampuni yake. Anadai kuwa Teknolojia ya Smartphone imesababisha yeye kupoteza muda mwingi kujibu Mails ambazo hazina umuhimu mais

Binti "akiharibika" arudishwa kwao....

...ambako hajawahi kuishi (hajakulia) huko maisha yake mapya ya "ukubwani hivyo kuwa Mgeni. Hii tabia mie huwa inanikera sana, enzi zile nakua nilikuwa nasikia tu watu wakisema "aah fulani, kashika mimba nimemrudisha kwao" au "amelimbukia sana maisha ya mjini, nimerudisha kwao". Unapochukua mtoto wa Mtu akiwa Mdogo kwa nia ya Kuishi nae kama "msaidizi" (which ni kinyume cha Sheria) au kukubali jukumu la kulea mtoto baada ya Wazazi wake kutangulia(Kufariki) unapaswa kuendelea kuishi nae na kumpa support/saidia ili arudi kwenye "mstari" sio kumpeleka "kwao" ambako ni Mgeni! Pia sio haki kwa watu wa kule "kwao" kubeba "Mzigo" ambao wewe Mlezi ndio uliyesababishwa kwa maana moja au nyingine. Unalea Binti tangu anamiaka, tuseme sita....tabia atakazokuwa nazo ni matokeo ya Malezi yako, hivyo ikitokea "kaharibika" Hatia ni yako, sio ya watu wa "kwao".