Maisha haya! Nimekumbuka 1996/97 Mauaji ya Mwembe Chai (siku mbuki vema na sitaki ku-google vilevile)! Siku chache baada ya Mauaji yale bado kulikuwa na Maandamano ya Siri ya "Waislamu wenye Hasira".....Kile kifo cha yule Kijana pale Mwembe chai akianguka LIVE baada ya kupigwa Risasi na Polisi (FFU sijui) akiwa amevaa shati la Bluu Mpauko(light Blue) kamwe haitonitoka Kichwani! Ni kifo cha kwanza nilishuhudia live(on Tv)!! Sasa bila kujua si tukaenda Kariakoo siku ya Ijumaa! Ile tumemaliza manunuzi si tukakutana na Waandamanaji na FFU...wakayaachia Mabomu ya "Machozi"....oh boy! Nilihisi Vita kuu ya Mwisho wa Dunia ambayo sina Uzoefu nayo ndio imefika!!! Kimbia, huku na kule mara Tukakutana na jamaa (sijui Katibu au Mlinzi, ila alikuwa Mhindi) Wa SSC pale Msimbazi, akatufungulia Mlango kwenye Jengo la Simba....akawa anaita akina Mama na Watoto waende kupata Huduma ya kwanza....hihihihi kunawishwa Maji Usoni(wasn't a laughing matter then)! Anyway! Baada ya hapo k...