Skip to main content

Posts

Showing posts from September 13, 2015

Wazungu wanajua Kupenda au wanaogopa kuonwa Wabaguzi?

Kama ulikuwa na Uzoefu mbaya na Wanaume/Wanawake wa Rangi yako hili ni Tatizo lako, na uzoefu wako mbaya haufanyi wanaume/wanawake wote wa jamii hiyo kutokujua Mapenzi/kupenda. Linapokuja suala la kupenda kila "individual" anapenda kivyake kulingana na labda Ubora/viwango atakavyo/alivyojiwekea kutoka kwa mtu anaetaka kumpenda(well huwezi kutaka kupenda, penzi linaibukaga tu popote) na pengine ni kutaka kujaribu ili kuona wa rangi hii wapoje kama sio "attraction"(sio kila mtu anavutiwa na yeyote, wengine wanavutiwa na watu wa jamii/rangi fulani tu). Ukiachilia mbali hayo hapo juu, pia Imani au "life situations" zinaweza kukufanya Ufunge ndoa na Mtu wa Taifa/Rangi nyingine (mostly Wazungu) ili kuboresha maisha Kiuchumi au kuapta Makazi ya Nchi fulani ambayo kutokana na Imani yako ni kuwa Utaishi maisha Bora zaidi.....au Status kama sio (hii haikuhusu wewe) kukimbia "Kacha" Maana wanawake Weusi wa Kijamaica au USA/Latino kwa DIRAMA a

Mama wa Nyumbani kujipenda/pendeza.....Nani anakupa Ari?

Kwa sie Wafanyakazi huwa ni kawaida kushindia khanga/Pjs mwisho wa Wiki kwasababu tunatilia kila siku tuendapo kazini. Lakini je ikitokea umeamua kuwa Mama wa nyumbani kwa Muda(mie) utakuwa upo hivyo siku zote Saba za Wiki kwa Muda wote Mpaka mtoto aanze Shule?. Ni rahisi sana kujisahau na kupoteza "utambulisho" pale unapokuwa una-deal na watoto muda wote. Unafubaa, na ikiwa Nguo zako nyingi zilikuwa Office like ndio kabisaa(nani anavaa kiofisi wakati yupo nyumbani?). Skinny Jeans nazo ni shughuli....! Hapo ndio kutafuta Ari kunajitokeza....ni vema kuwa/kupata/kupewa Ari(kuwa Ispired that is) kwa uHasi ama uChanya.....zote ni hisia na ukizipata pengine unaweza kuzitumia kufikisha ujumbe kwa watu wengine au ukaepuka na labda kujifunza kama sio kupata nafuu kuwa "aah am  not the only one then". Mfano: Kuna Binti mmoja Maarufu ambae Kijamii anaonekana kuwa na Mwenendo mchafu na ni Mfano mbaya kwa Mabinti wengine ambao wanakuwa "ispayadi

Namna ya Kuondoa Mdoa(Tetekuwanga) Usoni.....

....haraka! Najua kuwa unajua napenda ku-share kile ambacho nimejifunza na kwa sehemu kubwa ni kutokana na Uzoefu. Kwabahati mbaya niliugua Tetekuwanga(ililetwa na Schooler boy wangu). Kwasababu yeye ni Mtoto haikuwa mbaya kama mie Mtu mzima. Hii ndio nikawa naitumia Asubuhi na Usiku kama mbadala ya hiyo hapo chini Lancome Genifique ndio Serum yangu Kitambo. Mbaya zaidi Mapele yakajitokeza kwa Wingi Usoni( sijui kwanini hayakwenda Mapajani au Tumboni au Miguuni)....unapopata tatizo la Ngozi mahali ambapo sio rahisi kuficha inakupotezea Amani kabisa yaani. Hakuna Dawa ya kuondoa Mdoa hayo kwa haraka(inachukua Miezi 2 mpaka Miaka kadhaa inategemea madoa yapo deep kiasi gani Ngozini). Dactor niliandikiwa dawa ya kuondoa Madoa(mie naita Mkorogo) lakini baada ya siku chache nikahisi inaharibu ngozi yangu kwa namna nyingine, kwamba inaondoa Mdoa Meusi Usoni lakini "pores" zinapanuka/zinakuwa kubwa(sijawahi kuziona pores zangu) nikaamua kuachana nayo.