...nani Malaya? Hello there. Kwenye harakati za Mpito za Ujana ni wazi unajifunza kwa kufanya mambo mengi kwa kupatia au kukosea. Sio mara zote unakosea ili kujifunza(usifanye makosa makusudi kwa kisingizo cha kujifunza), wakati mwingine unakosea kwa Uzembe(kutokujali). Kama ilivyo kwenye kila kipindi cha " Mpito" mambo huwa magumu.....wakati mwingine mtu unajikuta unakata tamaa na kuamua kuwa LIWALO NA LIWE na hapo ndio maamuzi ya kizembe yanapojitokeza. Inaweza kuwa Pombe au Utumiaji wa madawa na Ngono Holela au vyote. Inawezekana kabisa kufanya hayo ni katika hali ya kutafuta "amani" au kuondoa "msongamano wa mawazo" na pengine ku-fit in na jamii inayokuzunguuka wakati huo wa Ujana wako. Kwaharaka haraka unaweza kudhani umepata "tiba" lakini katika hali halisi unajiongezea shida/majukumu kabla ya Muda wako. Sasa, kutokana na hali ilivyo siku hizi (Mambo ya Haki sawa sijui Usawa) inafanya mambo mengi ambayo awali yalifanyw...