....ila usipokuwa muangalifu kwenye kuchagua Rangi za Mavazi/Nywele hakika utaonekana Mchafu(huvutii), hii haina kujiamini.....nadhani ni muhimu kuchagua Rangi zinazoendana na Rangi ya Ngozi yako.
Mambo?!!
Kuna siku nipo na mishughuliko yangu ya ndani wakati Asali wa Moyo anatazama Mashindano ya Tenesi ya Wibledoni. Anapendezwa sana na wale Williams Dadaz....mmoja wao alikuwa anacheza. Mwenyewe anafurahia uchezaji wake (au kuona Tako kila kisketi chake kinapoinuka hihihihi maana mdada mMashallah).
Sina hili wala lile nasikia mwenznagu anawasifia wadada Williams kwa kutokuwa kama Celebs wengine.....mie nkasema hao sio ma-Celeb ni Sports Stars (kwa Kiswahili ndio tunasemaje vile?) ila Media inalazimisha kuwaweka kwenye Kundi la M-aceleb kitu ambacho sio haki kwasababu wapo walipo kutokana na kazi/kujituma kwaoo na sio kuonekana kwenye Tv au kuuza Haidthi kwenye magazeti au....oh well kwa Umalaya.
Katika kufunga maelezo yangu nikamalizia na....kiukweli mie siwaelewi kwanini hawa wadada, wanamahela lakini wanaonekana kama wachafu?......Nikaambiwa na asali wamoyo tena kwa kung'aka...."Usikufuru Dinah, unadhani wao waliomba kuumbwa hivyo?"....alaa!!
Nilichogusia sio Rangi zao bali muonekano wao kwa maana ya Mitindo na Urembo.....huenda ni Rangi ya nguo wanazochagua/vaa wakiwa nje ya Michezo yao, au pengine mitindo na rangi ya Nywele/Wings inafanya waonekana kama Wachafu.
Nikupe Mfano....kuna yule mnamuita Super Model "legend" Fiderine Iranga halafu kuna Super Model Flaviana Matata (in my head she is Top SuperModel). Wote ni Weusi sana lakini mmoja anaonekana kama vile Mchafu.....sio kwamba haogi la hasha! bali uvaaji( Rangi za nguo/Wigs) na Urembo ndio vinafanya aonekane hivyo nilivyosema (kwenye Picha).
Daaah!.,,,wiki iliyofuata si ndio Nkaumwa Tetekuwanga hihihihihi mwee. Gotta stop Jajing'i.
Babai.
Comments