Hiyaaaa! Leo si Halloween bana, wacha nami niungane nao kwa kuzungumzia Wafu. Jana tulikuwa (Mimi na Asali wa Moyo) tunaangalia Tv, mara Tangazo la Documentary ya Ebola (Ebola crisis) hilooo! Nkasema mie sipendi kuona/onyeshwa miili ya wafu hata kama imefunikwa(hifadhiwa vizuri), kama wameenda wameenda tu hata mkituonyesha haifanyi Ebola kuwa Hatari zaidi ya ilivyo! Mwenzangu akasema, "mie sielewi kwanini watu hupenda kwenda kutoa "Heshima" za mwisho wakitegemea kumuona Marehemu kwa mara ya Mwisho, marehemu ambae hawakuwa nae karibu kama Ndugu(wa Damu). Kwanini utake kumuona Mtu akiwa Maiti? Nikakumbuka Msiba wa Marehemu Kanumba(Mungu akuongezee heri huko uliko, Ameen), ambao sasa umekuwa (in my head) kama "model" ya Misiba ya MaCeleb wa Bongo kwa Uwingi wa watu....*whispering* nasikia MaCeleb wa Kibongo wanaombea nao wajekuzikwa na watu wengi kama huyo nliyemtaja! Walioshiriki walilalamika na wengine kukasirika kwanini hawakupewa nafasi ya "kumuona" ...