Kila Mwanamke ni Imara hiyo inajilikana na wala huitaji kujitanganza(kuwa chini ya Kundi fulani kuthibitisha hilo), pamoja nakusema hivyo wewe kama Mke bado ni Dhaifu/laini(Kimwili) na hakuna kosa mkimama kuwa mlaini(jivunie udhaifu wako). Kazi yako kubwa Duniani ni kuwa msaidizi wa Mumeo, kuleta uhai(kubeba Mimba na Kuzaa), kulea, kufundisha na kutunza Familia. Ili uweze kufanya hayo(niliyoyatajabhapo juu) unatakiwa kuwa umejitolesha kwenye nyanja nyingine ili kurahisisha Maisha yako kama Wewe, Mama na Mke. Unapaswa kuwa na uwezo wa kufanya baadhi ya vitu haraka na kwa ukamilifu bila uwepo wa mtu wa pili iwe Mumeo au Muuza Huduma. Je ni nyanja gani hizo? Dharura; Unaweza kujituliza, kutafakari kwa haraka na kufanya uamuzi kwa faida yako na familia badala ya kusubiri mpaka Mumeo apokee Simu/arudi. Uchumi; kuwa na Akiba ya Senti kwa mahitaji madogo madogo(ya ghafla) nje ya Bajeti ya Familia(kutoka kwenye zile anazokupa Mumeo), sio kila akikupa Pesa u...