Nimekaa hapa nakumbuka watu wote niliosoma nao Msingi na Sekondari kwa Majina yao yote Mawili(la mwanzo na la Mwisho).....nimeambulia kusisinzia.
Darasa Moja tulikuwa. Wanafunzi 200na! Tuligawanywa katika Mikondo 5 yaani A-B-C-D-E-F....shule kubwa ka' Kijiji....hiyo Msingi. Sekondari hatukuwa wengi sana Mikondo ilikuwa Minne.
Sasa mwanamke nkasema ngoja nipime uwezo wa akili yangu sehemu ya kutunza kumbukumbu....nimefeli yaani nimepoteza kumbukumbu hata Miaka 40 sijafika!.
Nikajipa Moyo; labda niagize picha za enzi za shule ili nikiona sura zao niwakumbuke vema, lakini hata hivyo sikupiga picha na kila mtu niliesoma nae kwahiyo haitosaidia. Yaani ndio basi tena.
Nimejisikia vibaya sana....yaani kupoteza kumbukumbu ya sehemu ya Maisha yako ndio inauma hivi?!!!
Kama ulisoma na mimi na unanikumbuka eeh! Drop me a line.
Babai...
Mapendo tele kwako...