Jambo!
Msita (Mdako), Dama, Marede, "Amina sasa naomba, turudiane...hayo yamekwisha kipenzi changu" yaani kuruka Kamba....don't you miss them au wewe ulikuwa wa Kishua unashinda kubebelea ma VHS ya akina Comando Kipensi....??
Usiseme ulikuwa unacheza Game, enzi hizo Bongo hakukuwa na Games za Tv achilia mbali PCs....Tv zenyewe zimechanganya 1994.
Nilikuwa mzuri sana kwenye Marede na Mdako(Msita kwa wale wa pande za Shinyanga na Mwanza). Nikikamata Jiwe kwenye Mdako sikosei....kwenye Marede kila Timu ilinitaka mimi (niligombaniwa).
Marede ya kujaza Chupa kwa mchanga niliipenda lakini sikuruhusiwa kuicheza kwasababu ya vumbi(Nilikuwa na Pumu). Ila nilikuwa naibia....kisha narudi ndani nimebanwa....kupumua siwezi....jicho limetoka ka' Ndula(unazijua Ndula weyeeeee)....hehehe.
Naishia kuonewa huruma na kupewa na kupewa ile Inhaler, kisha nakuwa nimerudishiwa Uhai.....Nashukuru Imeisha (sijabanwa Tangu nilipofikisha miaka 21).
...