Umewahi kujiuliza kwanini sisi Waafrika Mataifa Mengine ambayo ni Masikini kuwa pamoja na kuamini Mungu na kusali kwetu kote bado hakuna Maendeleo? Kwanini Mataifa hayo yanaendelea kuwa Tegemezi wa Nchi za Ulaya Magharibi na Marekani?(Wacha sababu za Kisiasa na Historia hapa sio mahali pake).... Leo hapa (kwako itakuwa Jana) Mimi na Asali wa Moyo tulikuwa tunajadili kuhusu Ubinafsi wa sisi wanadamu, tukafikia mahali tukakubaliana (kwa kawaida huwa hatukubaliani)! Wazungu ni Washenzi kote-kote na wengi wao hawaamini Mungu as in kusali kucha kutwa na kwenda kutoa Sadaka kanisani kila J'2 lakini linapokuja suala la kusaidia Binadamu wengine wenye Matatizo huwa mstari wa Mbele! Huenda hilo ndilo linalowafanya waendelee kufanikiwa, kwamba hawakai(kupoteza muda) kusali na kutegemea Mungu awashushie Mahela ili wawasaidie wengine au kukesha na kuomba ili Mungu awape Makazi wakimbizi mahali palipo na Vita. Wanafanya yote hayo kwa Vitendo.... kuna Maduka kibao ya Misaada ambapo watu hujitole...