Skip to main content

Posts

Showing posts from December 14, 2014

Je wee ni Muafrika Halisi?

Kwamba vizazi 9 vya pande zote mbili (baba/ yako, Babu/Bibi yako, Baba/Mama wa Babu/Bibi yako, Baba/Mama yake Babu/Bibi wa Baba/Mama yako na whoever kabla ya wote hao) vilivyopita kabla yako ni Waafrika Weusi asilia bila tone la Uarabu, Ujerumani, Ureno na Uingereza? Baada ya Obama wale Mchanganyiko wakaonyesha "rangi" yao, hasa wa huku....walikuwa wanaongea kwa uchungu na hasira kuwa wao sio Weusi bali ni Mixed, hawataki kutambuliwa kama Weusi bali Weusi na____!....Which was/is fair ila kwanini msubiri Mpaka wakati wa Obama?!!! Huwa nakerwa na tabia ya baadhi ya watu (hasa Mixed ambao U-mixed wao hauonekani bali Weusi wao) wanaopenda kusema "mie ni robo Mhindi,Nusu na robo Muingereza halafu Nusu Muafrika". Vita ya Ubaguzi kati ya Weusi Mixed na Real Weusi bado ipo na inaendelea kukua hasa baada ya "mapinduzi" ya Natura hair kwa African american aka Black peeps. Wale Real ndio wanahisi wanahitaji pongezi