Skip to main content

Posts

Showing posts from May 10, 2015

Adui mpende.....mpende adui yako.

Hivi wewe una adui? Kusema ukweli kabisa mie sina adui which means mie sio adui wa mtu yeyote.....oh hello! Kuna wakati unazungumza na watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki) na unakutana na suala la maadui......kwamba wanawazungumzia "maadui zao" na jinsi gani wanawachukia halafu unajiuliza imekuaje mpaka hawa watu wanakuwa na maadui? Adui yako anaweza kuwa mtu yeyote kuanzia nduguyo wa damu mpaka yule uliewahi kuchangia nae mwili lakini sasa ni HISTORIA iliyofutika . Sababu za hawa majamaa kuwa maadui zinayofautiana lakini chanzo mara zote (nidhaniavyo mimi) ni ukaribu wao kwako. Ndugu: Unajua Ndugu wa damu mnapokuwa watu wazima mnabadilika (mnakuwa) na ule ukaribu wenu hupungua kutokana na mmoja wenu kuishi maisha tofauti na  (mume au mke) wake. Baadhi ya ndugu huwa bitter wakidhani kuwa huwajali tena na badala yale unajali zaidi mkeo/mumeo na "familia yake".....ni kweli halafu sio kweli kwa kisingizio cha  utahama kwenu na kumfuata mwenza wako. Jam

Mvaa Vimini na mzaa ovyo....

....nani hajiheshimu? Mambo vipi? Uchaguzi umepita....maisha yameanza upya Jana na Pound imeshuka thamani. Maana Ijumaa ilishuti mpaka kufikia 2,900Tsh(why am i telling you this? Never mind). Kuna wakati mtu unachoka kujielezea na kuelewesha baadhi ya watu kuwa Mavazi ya mtu sio tabia na mavazi mafupi sio kielelezo cha mtu kutokujiheshimu. Natambua kuna tofauti ya ufupi wa mavazi kulingana na umri japokuwa umri sio sababu ya mtu kubadilisha style yake ambayo anadhani kuwa inampendeza kulingana na shape yake au kulingana na kuonyesha kilicho "perfect" ili kuondoa attention kwenye kile akionacho kuwa ni "imperfect" (miguu vs sura) hiihihihihi mie. Sasa unapomuita mvaa nguo fupi kuwa ni Malaya, hajiheshimu au Changudoa(uchangudoa ni kazi japo siiungi mkono) na kumtukuza mvaa mavazi marefu na ya kujificha(eti heshima) lakini ana watoto 3+ kutoka wanaume watatu tofauti unakuwa bwegelao(bongwa la mabwege). Kabla hujachukia au kuponda vazi la mtu ambalo unadhan